Home » » MASHUGA MAMI, NGOMA ZA USIKU VYANZO VIKUU MAAMBUKIZI YA VVU PWANI

MASHUGA MAMI, NGOMA ZA USIKU VYANZO VIKUU MAAMBUKIZI YA VVU PWANI

NGOMA za usiku, mila zilizopitwa na wakati sanjali na uwepo wa mashuga mami na mashoga imeelezwa kuwa ni moja wapo ya sababu zinazochangia kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi wilayani Kibaha mkoani Pwani kutokana na njia hizo kutumiwa kuwahonga fedha ama zawadi zingine vijana wa kike na kiume

Kwa mujibu wa takwimu za idara ya Ukiwmi zilizopo hivi sasa mjini Kibaha ni kwamba kiwango cha maambukizi kwa watu waliopata ushauri na kupima VVU mjini Kibaha kimepanda kutoka asilimia 7 saba  mwaka jana hadi asilimia 9.7  tisa pointi saba mwaka huu idadi ambayo imetajwa ni kubwa kuongezeka kwa kipindi kifupi cha mwaka mmoja.

Akizungumzia hali hiyo,Mratibu wa Ukimwi mjini Kibaha Siwema Cheru amesema idadi ya watu waliofika kwenye vituo mbalimbali vya afya na kupata ushauri kisha kupima kwa kipindi cha mwezi Januari  hadi Desemaba mwaka huu ni watu 6,850 kati yao waliokutwa na VVU ni 665 wanaume wakiwa ni 214 na wanawake 451 hivyo kufanya kiwango hicho kufikia asilimia 9.7. sawa na ongezeko la asilimia tatu ya mwaka jana.

Cheru amesema takwimu hizo ni zile tu zilizoripotiwa katika vituo vya afya na kwamba kuna uwezekano mkubwa wapo watu wengi wagonjwa wa VVU  ambao hawajajitokeza bado kwenye vituo hivyo kwa uoga ama kujinyanyapaa wenyewe na badala yake kuendelea kujiuguza nyumbani kwa kutumia dawa za asili.

Amesema mbali ya hayo,nyumba za wageni zimekuwa hazizingatii umuhimu wa kuweka mipira ya kujikinga yaani kondoms na zinaruhusu hata wenye umri mdogo na wasio wanandoa kutumia vyumba.

Mratibu huyo wa Ukiwmi mjini Kibaha Cheru amewaasa watu walioanza dawa za kufubaza virusi vya makali ya Ukimwi-(ARVS) kuacha kusitisha dozi na kuendekeza ngono ili kuepuka sugu wa ugonjwa huo sambamba na kunyemelewa na magonjwa mbalimbali yanayopelekea vifo.

Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha ,Hajat Halima Kihemba amesema kuna kila sababu ya watu kujitambua na kushirikiana Serikali kupambana na maambukizi mapya ya VVU,kukomesha unyanyapaa kwa wanaoishi na Ukimwi na kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa