MAAFANDE
wa JKT Ruvu wenye makazi yao mkoani Pwani wametumia makosa ya kufanya
vibaya mzunguko wa kwanza ligi kuu bara kama darasa la kujifunza mbinu
mpya kuelekea ngwe ya lala salama inayotarajia kuanza januari 25
mwakani.
Kocha
mkuu wa klabu hiyo, Mbwana Makata amesema kikosi chake ni kizuri,
lakini kilikuwa na mapungufu kadhaa, hivyo akaamua kuongeza wachezaji
muhimu katika dirisha dogo la usajili liliofungwa septemba 15 mwaka huu.
Makata
aliwataja wachezaji wake wapya kuwa ni beki mwenye uzoefu mkubwa Chacha
Marwa, wengine ni Sino Augustino, Idd Mbaga na Cecil Luambano.
“Cha
msingi mzunguko wa pili unahitaji wachezaji wa kuja kufanya kazi na sio
wa kufundishwa mpira. Unatafuta wachezaji wenye uzoefu na ndio maana
tumemchukua Marwa. Ukimwangalia katika mazoezi yetu, anaonesha kiwango
kizuri cha kutusaidia”. Alisema Makata.
Kocha huyo aliongeza kuwa wiki ijayo wanaanza kucheza mechi za kirafiki ambapo kwa mujibu wa mipango yake atacheza mechi tano.
“Nikishamaliza
mechi za kirafiki, nitaweza kupata cha kuzungumza zaidi. Nitaelewa
mapungufu ya kikosi change na kujua wapi nielekeze nguvu zaidi”.
Alisema Makata.
Makata
alisema kuwa mipango yake ni kuunda kikosi ambacho kitacheza mpira kwa
pamoja `Team work` tofauti na mzunguko wa kwanza ambao timu ilipoteana
na kuambulia matokeo mabaya, licha ya kuanza kwa kasi na kuongoza ligi
kwa muda.
Aidha,
kocha huyo mwenye uzoefu wa soka la Tanzania, aliwaomba mashabiki wao
wa Pwani na nje ya Pwani kuiunga mkono timu yao kwa hali na mali.
“Popote
pale duniani, mashabiki ni nguzo ya timu kupata mafanikio. Wengine
wanawaita mchezaji wa 12. Ni nafasi kwa mashabiki wetu kuiunga mkono
timu yao ili ifikie malengo iliyojiwekea”. Alisisitiza Makata.
JKT Ruvu ilianza mzunguko wa kwanza kwa kushinda mechi tatu za mwanzo na kukaa kileleni kwenye msimamo.
Mashabiki
walidhani imedhamiria kuzimaliza Simba, Yanga, na Azam fc, lakini mambo
yakawaendea doro na kuanza kuchezea vichapo vingi.
Mpaka
mzunguko wa kwanza unamalizika, JKT Ruvu ilikuwa imeshinda mechi tano
(5), haikutoka sare yoyote na kufungwa mechi nane (8), hivyo kumaliza
katika nafasi ya tisa (9) kwa kujikusanyia pointi 15.
Na Baraka Mpenja
Tel: 0712461976 au 0764302956
Chanzo;Fullshangwe blog
0 comments:
Post a Comment