Mahiza alitoa wito huo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema kumezuka wimbi la kuibiana mifugo migogoro ambayo inaashiria uvunjifu wa amani ndani ya Mkoa huu.
Bila kuwataja wafugaji kuwa wanatoka katika jamii gani Mahiza alisema
wafugaji kwa wafugaji wamekuwa wakiibiana mifugo ikiwa machungani na
katika kukabiliana na jambo hilo wamekuwa wakitumia silaha za jadi
kutaka kuanzisha mapigano.
Alisema ofisi yake imesaidia kutuliza vurugu ambazo zilitaka kuanza
kufuatia wizi huo, ambapo aliwaonya wafugaji hao kuachana na tabia ya
kuwaagiza watoto kwenda na ng’ombe machungani.
“Wafugaji wanapowatuma vijana wadogo kwenda machungani wawe
waangalifu kwa kipindi hiki inatakiwa waende watu wakubwa kuchunga
ng’ombe wakati vuguvugu hili la wizi wa ng’ombe likiwa ndio tumelizima
ili tujue kama limekwisha wasiwaachie watoto kubaki na ng’ombe
maporini,” alisema Mahiza.
Alitoa rai kwa wafugaji wanaojijua hawako kihalali mkoani hapa
wasiendelee kuwepo na wale ambao wapo kihalali wahakikishe
hawawakaribishi wafugaji wenzao ili kupunguza ongezeko la mifugo.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment