Home »
» Wanafunzi 200 wasoma darasa moja
Wanafunzi 200 wasoma darasa moja
|
|
|
|
SHULE ya Msingi Kongowe wilayani Kibaha, Pwani, inakabiliwa na
uhaba wa madarasa jambo linalosababisha wanafunzi 200 kukaa katika
darasa moja.
Akielezea changamoto za shule hiyo wakati wa kukabidhiwa mabati 40 na
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani, mwalimu mkuu wa shule
hiyo, Beatus Lingumbuka, alisema shule hiyo kwa sasa inahitaji vyumba
nane vya madarasa, ili kukabiliana na changamoto hiyo.
“Halmashauri inatujengea chumba kimoja na wananchi wanajenga vyumba
viwili, hapa inahitajika msaada zaidi, kwani katika halmashauri ya mji
wetu wa Kibaha hakuna shule yenye mlundikano mkubwa wa wanafunzi kama
hii,” alisema.
Alimshukuru meneja wa TRA kwa kuwasaidia mabati hayo na kofia za
kujengea ambazo zitasaidia kuezeka vyumba vya madarasa vinavyojengwa na
wananchi na kuwezesha wanafunzi kuvitumia.
Meneja wa TRA mkoani Pwani, Highness Chacky, alisema wametoa msaada
huo baada ya kupata taarifa ya changamoto ya shule hiyo na kuamua
kutumia Wiki ya Mlipakodi kufikisha msaada huo.
Mbali na msaada huo, vifaa tiba pia vilitolewa katika Wilaya ya
Mkuranga, na Shule ya Msingi Kiluvya ilisaidiwa ukarabati wa darasa
lililoezuliwa na mvua.
Katika hatua nyingine, gazeti la Tanzania Daima na Radio Clouds
walipata vyeti kutokana na kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa
na mamlaka hiyo mkoani Pwani. Pia washindi watatu kutoka kila wilaya
walipata vyeti kutokana na kutokuwa wasumbufu katika zoezi la kulipa
kodi.
Chanzo;Tanzania Daima
|
|
|
0 comments:
Post a Comment