Home »
» MAHIZA AVALIA NJUGA MIGOGORO YA MIPAKA BAGAMOYO
MAHIZA AVALIA NJUGA MIGOGORO YA MIPAKA BAGAMOYO
Katika
hatua inayodhihirisha Mkuu waMkoa wa Pwani, BI.MWANTUM MAHIZA
ameamua kuchukua hatua za makusudi katika kukabiliana na migogoro ya
mara kwa mara kati ya wafugaji na wakulima katika eneo la CHAMAKWEZA
na PINGO wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani amechukua uamuzi mgumu wa
kutembea jiwe hadi jiwe la mpaka.
Ilimlazimu
Mkuu huyo wa mkoa BI.MAHIZA kutembea takriban kilometa 13
akiambatana na maofisa ardhi kutoka idara ya ardhi Bagamoyo ili
kutafuta mawe ya mpaka unaoonyesha jinsi eneo hilo lilivyogawanya,
na Chamakweza kwa wafugaji na Pingo kwa wakulima.
BI.MAHIZA
katika ziara hiyo ya kukagua mipaka ya vijiji hivyo ameshuhudia
mwenyewe jinsi ya wananchi ambao hawana nia nzuri na juhudi
mbalimbali za usuluhishi zilizofanywa awali kwa kung’oa mawe
yanaonyesha mipaka ya vijiji hivyo viwili vilivyopo katika mgogoro
huo kwa karibu miaka 20 sasa.
Mkuu
huyo wa mkoa wa Pwani amesisitiza kuwa makubaliano ambayo yalifikiwa
awali ya kuweka mipaka kutenganisha maeneo hayo kwa misingi ya
ufugaji na ukulima yaheshimiwe na hasa ikizingatiwa kuwa wajumbe
waliofanya maamuzi hayo wanatoka pande mbili zinazokinzana za
wakulima na wafugaji.
BI.MAHIZA
amewataka wananchi wa pande zote mbili yaani wakulima na wafugaji
kujenga desturi ya kuheshimiana kwa manufaa ya ustawi wao na
maendeleo ya vijiji husika.
0 comments:
Post a Comment