Madereva wa Magari madogo ya
mizigo,na Pikipiki aina ya Toyo na Bajaj wamefanya maandamano ya amani kuelekea
ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Kibaha kushinikiza kuwekewa kwa
miundombinu katika eneo ambalo wanafanya shughuli zao.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi akizungumza na mmoja wa Viongozi wao, BW.ABDALLAH ZANDA amesema kitu
kikubwa kilichowafanya wachukue hatua ya kuandamana ni Polisi kuwakamata wakiwa
wanatekeleza majukumu yao ya kila siku.
BW.ZANDA amebainisha kwa kipindi
kirefu halmashauri walitoa agizo la magari na pikipiki za kubeba mizigo kuhama
eneo hilo, jambo ambalo wao kwa upande wao hawana kipingamizi nalo, lakini
tatizo ni kukosekana kwa miundo mbinu ya uhakika katika eneo hilo.
Amefafanua baadhi ya vitu muhimu
ambavyo vinakosekana ni pamoja na huduma ya choo katika sehemu ambayo inakaa
karibu watu 100, mabanda ya mamalishe, kukosekana kwa mabanda ya kupumzikia
madereva na wateja na hivyo kuonekana halmashauri kama imekurupuka kuanzisha
zoezi hilo.
Ofisa mipango halmashauri ya mji wa
Kibaha, BW. JOHNSON NYAMITI amewataka madereva wa magari madogo ya mizigo na
pikipiki hao kuwa watulivu na ameshukuru kukutana nao na kuwaahidi yale ambayo
yoyote wameyalalamikia yatapatiwa ufumbuzi.
BW. NYAMITI amewaasa madereva kuwekwa
kwao pale wasjichukulie kama wametelekezwa bali halmashauri inafahamu uwepo wao
na itahakikisha inaweka kifusi eneo hilo ili liweze kutumika kipindi chote cha
Mwaka.
0 comments:
Post a Comment