Home » » Vijiji vya Bagamoyo kunufaika na Umeme wa Jua

Vijiji vya Bagamoyo kunufaika na Umeme wa Jua


Kipozi akifungua mafunzo
Mkuu wa  Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi akifungua mafunzo.
Mhandisi Magessa akielezea mfumo huo wa jua
Mhandisi Magessa akielezea mfumo huo wa jua kwa washiriki.
moja ya vifaa walivyotengeneza wakufunzi walipokuwa wakijifunza
Moja ya vifaa walivyotengeneza wakufunzi walipokuwa wakijifunza.
Ally Jakaya akifanyiwa interview
Ally Jakaya akifanyiwa interview.
Na Andrew Chale, Bagamoyo
Mkuu wa  Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi  amewataka wananchi wa wilaya hiyo hasa vijijini kuchangamkia fursa ya  kuweka  umeme nuru  utokanao na jua maarufu kama Solar, ilikuboresha maisha yao na maendeleo kwa ujumla.
Kipozi  amesema hayo mjini Bagamoyo wakati wa hafla ya kufungua mafunzo maalumu ya umeme huo kwa mafundi umeme, wadau na wauzaji wa vifaa vya umeme na vijana mbalimbali ndani ya wilaya hiyo ambapo mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Akielezea  kufarijika na mafunzo hayo ndani ya Wilaya yake, Kipozi amesema “Ni fursa ya kipekee kwa  washiriki kutumia ujuzi huu kwani utaboresha maisha yenu na  pia kwa vijiji  vitanufaika na umeme huu wa nuru” amesema.
Na kuongeza kuwa, kwa fursa hiyo anaamini matumizi ya kukata miti  hovyo yatapungua na baadala yake wananchi watanufaika na huduma hiyo endapo wataichangamkia.
“Nawaomba wananchi hasa mulio vijijini kuchangamkia fursa hii ya umeme nuru, pia nawapongezeni wakufunzi na wandaaji kwa  kuja muda muafaka   kwani mafunzo haya ni mipango endelevu ambayo itasaidia kusambaza teknolojia  ya nishati mbadala vijijini sambamba na kuwahamasisha wananchi kutumia nishati zitokanazo na teknolojia  ya nishati  jadilifu” alimalizia Kipozi.
Kwa upande wake, mkuu wa mafunzo hayo ya umeme nuru,  Mhandisi, Finiasi Magessa alisema mafunzo hayo yatasaidia kuboresha maisha ya watanzania mbalimbali hasa wa vijijini  ilikufikia malengo ya MKUKUTA, ili kila Mwananchi apate umeme wa uhakika na gharma nafuu ifikapo 2015.
Aidha, wanamafunzo wanatarajia kufaanya kwa vitendo  kwa kufunga  umeme nuru katika shule  na nyumba za walimu za  Sekondari Kiwangwa, Matipwili na Kibindu, huku mafunzo hayo yakitaraajia kumalizika Novemba Sab, mwaka huu.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa