MKAZI wa kitopeni
Lushoto Mkoani Tanga Ibrahim Bakari maarufu kama Semkumba,(36) anashikiliwa na
jeshi la Polisi mkoani Pwani kwa kosa la kukutwa na noti bandia 304 za shilingi
elfu 10 zikiwa na namba tofauti zenye thamani ya mil. 3,040,000
Kamanda wa Polisi
mkoani humo,Ulrich Matei amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa jana majira ya jioni
huko Chalinze wilayani Bgagamoyo wakati akijaribu kununua maji kwa kutumia noti
moja wapo kati ya hizo kwa mfanyabiashara ndogo ndogo wa eneo hilo.
Amesema muuzaji wa maji
huyo alipata mashaka juu ya uhalali wa noti hiyo na kutoa taarifa kwa askari
waliokuwa jirani ambao walimfuta kijana huyo na kumkamata kisha kumfanyia
upekuzi na kukuta noti zingine 304 zikiwa zimehifadhiwa kwenye bahasha tatu
tofauti kwenye begi lake.
Kamanda huyo alisema
utaratibu huo wa kutumia noti bandia ni hatarishi kwa uchumi wa nchi na
hata mtu mmoja mmoja na hivyo jitihada zaidi za kuwabaini wanaohusika na
mtandao huo zinafanyika sambamba na kusaka mashine zinazozalisha fedha hizo
feki.
Katika tukio jingine
mkazi wa Kitonga Rufiji Hamis Omary maarufu Chinga (15) amefariki dunia baada
ya kukamatwa na mamba kisha kuraruliwa sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo
kichwa,wakati akiteka maji kwenye mto Rufiji.
Matei amesema tukio
hilo limetokea majira ya saa nane mchana jana na mwili wa marehemu umekutwa
ukiwa baadhi ya viungo vimenyofolewa ikiwemo mkono na mguu wa kushoto na
kutupwa umbali wa km 4 toka eneo la tukio ndani ya mto Rufiji na tayari maiti
imefanyiwa uchunguzi wa daktari na kukabidhiwa kwa ndugu kwa mazishi.
0 comments:
Post a Comment