MKAZI wa Kijiji cha Mlongazila, wilayani Kisarawe,
Pwani, Moshi Hamad anatuhumiwa kumng’ata mwanaye, Khadija Hamad (6) sehemu za
siri kwa madai ya kujisaidia haja kubwa na ndogo hovyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Tanzania Daima
juzi wilayani Kisarawe, wakazi hao walisema mama huyo amekuwa na tabia ya
kumfungia ndani mtoto wake huyo na kumchapa kwa zaidi ya nusu saa, akitumia
nyaya za simu na kumng’ata sehemu mbalimbali za mwili zikiwamo za siri na
kumsababishia maumivu makali.
Wakazi hao walisema waliamua kutoa taarifa kwenye
dawati la haki za binadamu baada ya kuchoshwa na vitendo hivyo, na sasa
wamelitaka Jeshi la Polisi kumkamata mama huyo na kumchukulia hatua.
Stella Musa, alisema sehemu za siri za mtoto huyo
zimeharibiwa kutokana na kung’atwa na meno, huku zikiwa na vidonda vinavyodaiwa
vimetokana na kuchomwa na kitu chenye ncha kali.
“Wazazi wa mtoto huyo ni wanangu, siku moja mama
huyo alimuumiza mkono. Nilimchukua na kukaa naye nyumbani kwangu kwa mwezi
mmoja nikimuhudumia kwa kumkanda kwa maji ya moto,” alisema Stella.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Mlongazila, Paulo Idana
ambaye pia ni katibu wa dawati la kutetea haki za binadamu, alisema suala hilo
limewafikia, hivyo wanachukua hatua za kisheria huku mtoto huyo amewekwa chini
yao kwa matibabu zaidi.
“Tulimfuata mama huyo Septemba 20 mwaka huu na
tulifanya nae mahojiano mbele ya ofisa mtendaji wa kijiji na alikiri akisema
alifanya hivyo kwa sababu ya hasira. Tunafanya utaratibu ili tumfikishe kwenye
vyombo vya sheria,” alisema Idana.
Akieleza mkasa huo, mtoto huyo alisema wakati
mwingine mama yake alikuwa akimwita ili amfundishe kusoma na aliposhindwa
aling’atwa mgongoni, mapajani na sehemu za siri huku akisema atamfanyia hivyo hadi
ajue kusoma.
Mama wa mtoto huyo, Moshi, alisema alikuwa akitoa
adhabu kwa mwanaye huyo kutokana na kujisaidia haja ndogo na kubwa hovyo wakati
akirudi shule.
“Nafanya hivi kutokana na hasira siwezi nikamuona
mtoto wangu anajisaidia haja kubwa na ndogo kwenye nguo nikamwacha tu, lazima
nimwadhibu… jana alitapika kwenye sahani. Je, mtoto kama huyu nitamwacha?”
alihoji Moshi.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Khadija Samizi
alikiri kuwepo kwa tukio hilo
0 comments:
Post a Comment