GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (B.o.T), Profesa
Benno Ndulu amesema Watanzania wanapaswa waelewe kwamba kukua kwa uchumi
hakumaanishi ndiyo mwisho wa matatizo yote nchini.
Alisema kuwa kasi ya kudhibiti mfumuko wa bei
inaendelea vizuri ikilinganishwa na miezi 18 iliyopita ambapo mfumuko ulikuwa
ni zaidi ya asilimia 19.
Prof. Ndulu alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua
semina ya kuwajengea uwezo na ufahamu waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali
juu ya kuandika habari za biashara na uchumi inayofanyika mjini Bagamoyo.
‘Tunaamini mfumuko wa bei nchini utaendelea
kupungua kwa kiasi kikubwa licha ya baadhi ya nchi duniani kuendelea kuwa
katika jitihada za kujikwamua na mdororo wa uchumi,” alisema.
Kuhusu akiba ya fedha za kigeni, Prof. Ndulu
alisema B.o.T ina akiba ya kutosha kuweza kukabiliana na hali yoyote ya dharura
kama itajitokeza.
Alisema hali ya kiuchumi katika nchi tajiri za
Ulaya bado ni tete na hata zile nchi zilizokuwa zikiinukia kwa ajili ya
kuhakikisha dunia haiathiriwi kwa wakati mmoja na hali hiyo, zimeanza kurudi
nyuma kutokana na kuwa na matatizo madogo madogo.
Alizitaja baadhi ya nchi hizo zinazoinukia kiuchumi
na ambazo zimeanza kuwa na matatitzo madogo madogo kuwa ni Brazil, India, China
na Indonesia.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment