WAKAZI
wa Mkoa wa Pwani wametakiwa kuwa makini kwa kukipa kura Chama Cha
Mapinduzi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika
mwaka 2014 li kiweze kuendelea kutekeleza ilani kwa kutimiza mahitaji ya
wananchi wake katika maeneo mbalimbali.
Wito
huo umetolewa jana mjini Kibaha na Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani Sauda
Mpambalyoto wakati akiongea na wanachama wa jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT)
kata ya Tumbi kwenye mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya mke wa mbunge wa jimbo
la Kibaha mjini.
Mpambalyoto
aliwataka wananchi kutobadilika na badala yake kubaki na msimamo wao wa
kuendelea kukipa kura chama hicho ambacho kimeonyesha mabadiliko makubwa kwa
kuwaletea maendeleo katika Nyanja mbalimbali.
Aidha
amewataka wananchi wa mji wa Kibaha kuwa karibu na mbunge wao pale wanapoona
kuna changamoto inawakabili ili iweze kutatuliwa kwa haraka na kuendelea
kufanya mambo mengine ya kimaendeleo.
Kwa
upande wake mke wa mbunge wa jimbo hilo Selina Koka amesema kuwa
aliwataka wanawake kutojibweteka na badala yake kuendelea kushirikiana katika
mambo ya ujasiriamali ambayo yatawasaidia kuondokana na hali ya utegemezi .
Koka
katika mkutano huo ameahidi kuchangia shilingi million 2.5 kwenye matawi matano
ya kata hiyo ili wanawake waendelee kujiinua kwenye shughuli za ujasiriamali na
kuwaahidi kuendelea kushirikiana nao pale wanapokua na matatizo kwenye vikundi
vyao.
Kata
hiyo inawanachama 557 wa UWT , inakabiliwa na changamoto ya kutokua na ofisi ya
UWT ya kata, pamoja na baadhi ya wanachama kutokua na mwamko wa kulipia kadi
zao kwa wakati na hivyo kufanya idadi ya wanachama hai kuwa 272.
0 comments:
Post a Comment