SERIKALI imeendelea kuwasisitizia
Wazazi na wanafunzi mashuleni kuwa wanafunzi wote 136,000 waliofeli kidato cha
pili mwaka jana na kutakiwa kurudia darasa hilo wanapaswa kufanya hivyo bila
kushurutishwa na kwamba wasijidanganye kuwua watafanya mitihani ya kumaliz
akidato cha nne mwakani kwani namba zao hazipo.
Pia wanafunzi hao wasije
wakarubuniwa na baadhi ya walimu wakuu wa Sekondari nchini kuwa licha ya kufeli
kwao wanaweza kuendelea na kidato cha tatu mwaka huu kwani hawataweza kufanya
mitihani ya Taifa ya kidato cha nne mwakani kama wanavyodhani kutokana na namba
na majina yao tayari zimeondolewa katika orodha hiyo ya mwakani.
Tahadhari hiyo imetolewa jana na
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo wakati akifungua
mafunzo ya Waratibu Elimu kata Kitaifa yanayoendeshwa na Wakala wa Maendeleo ya
Uongozi wa Elimu (ADEM) huko Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Mulugo amesema ana taarifa ya
kuwepo kwa baadhi ya wanafunzi kati ya hao 136,000 ambao wameshawishiwa na
Wakuu wa shule pamoja na wazazi wao kadhaa kuendelea na kidato cha tatu kwa
matumaini ya kuwa watafanya mitihani ya kumaliza kidato cha nne mwaka ujao
imani ambayo Waziri huyo alisema itakuja kuwaliza baadae maana kundi hilo
halina nafasi ya kuhitimu mwakani.
Kutokana na hali hiyo Naibu
Waziri Mulugo amewaagiza Waratibu Elimu Kata nchini wafatilie mara moja
wanafunzi wote wa kidao cha pili waliofeli kama wamekariri darasa hilo kama
ilivyoagizwa na Wizara na endapo watawabaini waliokaidi na kuendelea kidato cha
tatu mwaka huu watoe taarifa mapema ili hatua za kisheria zichukuliwe
dhidi yao na walimu waliohusika na udanganyifu huo,
Awali Afisa Taaluma wa Mkoa wa
Daresalaam Benadeta Thomas amesema mafunzo hayo ya waratibu elimu kata Kitaifa
yanaendeshwa katika mikoa 11 nchini na ni utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya
Elimu ya Sekondari ngazi za kata na kwamba mikoa hiyo ni Daresalaam, Mbeya,
Morogoro,Mtwara,Kilimanjaro,Singida,Ruvuma,Arusha,Tabora, Mwanza na Tabora
Benadeta ameongeza kuwa waratibu
elimu kata hao pamoja na majukumu mengine waliyonayo sasa wanaanza kuwajibika
kusimamia na kufatilia kwa karibu utoaji wa elimu ya sekondari katika ngazi ya
kata ikiwemo kufatilia matumizi ya fedha na vifaa vya kufundishia na kufatilia
na shughuli za ujenzi na ukarabati wa miundombinu mashuleni.
0 comments:
Post a Comment