Home » » News alert: Mfanyakazi taasisi ya utafiti Bagamoyo abakwa na kunyongwa mpaka kufa

News alert: Mfanyakazi taasisi ya utafiti Bagamoyo abakwa na kunyongwa mpaka kufa

MFANYAKAZI anayedaiwa ni mtumishi wa taasisi ya utafiti wa malaria tawi la Bagamoyo Mkoani Pwani ,amekutwa ameuawa kikatili chumbani kwake baada ya kubakwa kisha kunyogwa na mtu anayedhaniwa kuwa ni mpenzi wake huku chanzo cha kufanyiwa unyama huo kikiwa hakijajulikana.

Msichana huyo mwenye umri wa mika 33 (jina tunalihifadh) anadaiwa kuuawa kikatili Jumamosi mwishoni mwa wiki iliyopita majira ya saa 12 jioni nyumbani kwake eneo la Majani Mapana wilayani humo.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa ofisi yake imepata taarifa za kunyongwa msichana huyo kutoka kwa wapangaji wenzake na walienda kwenye nyumba hiyo walithibitisha tukio hilo

 Awali wakizungumza na wilayani humo mmoja ya wapangaji wenzake na marehemu Fauzia Abdalaha(20) wamesema mara ya mwisho kumuona msichana huyo ni siku ya Ijumaa jioni ya tarehe 19 mwezi huu ambapo mida hiyo walimsikia akizungumza na simu  na kumtaka mtu aliyekuwa akiongea naye amsubiri ili waweze kuonana na kuzungumza.

 Mpangaji huo ameongeza kuwa muda mfupi baada ya dada huyo na mtu huyo kuingia  katika chumba chao alisikia wanabishana lakini hakuweza kujua wanabishania kitu gani na ndiyo hawakumuona tena mpaka walipokuja kugundua kuwa ameuawa kikatili majira ya saa saba mchana Jumamosi hivyo kutoa taarifa Polisi

Fauzia amesema kuwa kilichowafanya kutomfuatilia kwa siku hiyo ni kutokana na tabia za binti huyo kuwa msiri na mkimya sana na mtu ambaye alikuwa hapendi kujichanganya na wenzake kwani mara nyingi amekuwa akishinda ndani kwake tu baada ya kusalimiana .

 Naye baba mkubwa wa marehemu Mtoto Sulemain amesema kuwa kiujumla familia imepatwa na mshtuko mkubwa sana kutokana na kifo hifo cha ghafla na cha kikatili kilichompata binti yao na kuiomba Serikali kuhakikisha inafanya jitihada zake zote kuweza kumfikisha mahakamani mhusika.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa