MBUNGE wa Kibaha Mjini, Silvesrty Koka (CCM), amemjia juu Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji huo, Jenipher Omolo, kwakumtaka aache tabia ya
kuwaonea madereva wa pikipiki maarufu bodaboda. Mbunge huyo, alidai
Omolo amekuwa akiwatoza fedha nyingi waendesha bodaboda kwani kufanya
hivyo ni sawa na unyonyaji.
Koka, alitoa kauli hiyo jana, wakati akizungumza na umoja wa wamiliki na madereva wa pikipiki uliofanyika kwa kuwashirikisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jeshi la Polisi na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Hajjat Halima Kihemba.
Alisema madereva wengi wa pikipiki wametoka katika mazingira magumu, huku wengine wakitoka katika vikundi vya uhalifu, wanatakiwa kusaidiwa badala ya kuwakandamiza.
Alisema hivi sasa, mkurugenzi huyo ameweka kiwango cha tozo ya faini ya Sh 120,000 ambayo dereva wa pikipiki anapaswa kulipa pindi atakapokamatwa na kosa.
Alisema kiwango hicho, ni kikubwa mno na kinatakiwa kupunguzwa haraka iwezekanavyo.
"Nasema lazima mkurugenzi akae na kuangalia upya kodi za madereva wa pikipiki kwani fedha wanazotozwa hivi sasa ni uonevu mkubwa kwani kiwango cha Sh 120,000 ni kikubwa hali ambayo itawafanya wengi wao kurudi kule kwenye ukabaji na kama hatashindwa kutekeleza agizo langu, mimi nitalivalia njuga,'' alisema Koka.
Hata hivyo pamoja na mambo mengine, mbunge huyo aliwataka madereva wa pikipiki kuhakikisha wanatumia vyema sheria za barabarani, ili kuondokana na ajali zinazotokea mara kwa mara.
CHANZO GAZETI LA MTANZANIA

0 comments:
Post a Comment