Matumizi ya mtandao
yamekuja na changamoto zake ambazo zimesababisha kasi mpya ya mmonyoko wa
maadili katika jamii, kutokana na baadhi ya watu kutumia mitandao hiyo kinyume
na taratibu zinazongatia ustaarabu na maadili.
Katika tukio moja lililotokea
jana mwanadada mmoja (Jina tunalihifadhi) mkazi wa mjini Kibaha amejikuta
katika wakati mgumu kufuatia rafiki yake ambaye amesoma nae shule ya msingi
kumchafua kupitia mtandao wa kijamii PEPERONITY.
Binti anasema kijana
huyo ambaye amefanya hivyo anamkumbuka kwa jina moja la BARAKA ambaye kwa sasa
anaishi Mwanza ambaye kwa mara ya mwisho alikutana naye Kituo cha Mabasi ya
mkoani Ubungo ambapo kijana huyo alimuomba namba yake ya simu.
Na wakati
wakibadilishana namba hizo, Kijana alimuuliza Bint. Shaaban kama ameshazaa na
alipojibiwa ndipo alipoaanza kumwambia maneno ya kuudhi na kejeli na kumuahidi
kuwa atamkomesha, na ndipo jana ghafla akaanza kupokea simu kutoka kwa wanaume
wakware.
Ameongeza kuwa mara
akaanza kupokea simu kutoka kwa watu mbalimbali wakitaka kukutana nae kwa lengo
la kufanya nao mapenzi kama alivyojitangaza na kuweka namba yake ya simu ya
PEPERONITY ili watakaomhitaji wampigie.
Amefafanua kuwa
alipowauliza wamepata wapi namba yake ya simu, alijibiwa wameipata katika
mtandao huo wa PEPERONITY ambao unajishughulisha na mambo yanayohusiana na
ngono kwa kiasi kikubwa, na hivyo kuwa na wakati mgumu kutokana muda wote
kupigiwa simu na watu wenye mahitaji ya ngono.
Kutokana na hali
hiyo, binti aliamua kwenda kituo kidogo cha Polisi Mailimoja mjini Kibaha na
kutoa maelezo na huku juhudi zikifanyika kumtafua anayehusika na udhalilishaji
huo wa kijinsia.
Baadhi ya watu niliongea
nao kuhusiana na kadhia hiyo, BW. JOHN GAGARIN ameishauri jamii kutumia
mitandao ya kijamii kwa manufaa badala ya kuchafuana
Naye Kessy GABRIEL
mkazi wa Maili moja mjini Kibaha ameitaka TCRA kupambana na vitendo vyote vya
matumizi yasiyofaa ya mtandao ili kuepusha usumbufu kwa raia wema
unaosababishwa na baadhi ya watu wenye itikadi hasi.
0 comments:
Post a Comment