TABIA ya baadhi ya watu kuchafua
mazingira kwa kuchoma moto nyasi ama mazao yao yaliyopo kando ya barabara kuu
imesababisha vifo vya watu wawili huku wengine zaidi ya 30 wakinusurika kifo
katika barabara ya Rufiji Lindi jirani kabisa na daraja la Mkapa wilayani humo.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa
Polisi mkoani Pwani Yusufu Ali amesema watu wawili Abdalah Said (30) mkazi wa
Umwe na Yahaya Shamte (35) mkazi wa Mgomba Ikwiriri wamekufa papo hapo
baada ya kugongwa na basi mali ya kampuni ya Najma wakati walipokuwa wakisafiri
na pikipiki kwenye barabara hiyo.
Kamanda Ali amesema wakati wa
tukio hilo kulikuwepo na moshi mkubwa uliotanda eneo kubwa inalozunguka
barabara hiyo katika kijiji cha Kwangayoga hali ambayo ilimsababisha dereva wa
pikipiki T 600 CBD aina ya Sunlg kushindwa kuona mbele vizuri na hivyo kukutana
uso kwa uso na basi T 599 CBL aina ya Youtong mali ya Najma iliyokuwa ikiedeshwa
na Said Ali(40).
Amesema ajali hiyo ilikuwa mbaya
kwani marehemu waliburuzwa katika lami na miili yao kusagika vibaya huku mmoja
akikatika kichwa na kwamba chanzo cha ajali hiyo ni moshi huo wa moto na kwamba
tayari dereva wa basi anashikiliwa na Polisi.
Katika hatua ingine raia watatu
wa Ethiopia wanashikiliwa na Polisi Pwani kwa tuhuma za kukutwa wakiwa
wameingia nchini bila kuwa na kibali kwa kutumia njia ya usafiri wa baharini
kutoka nchini Kenya.
Kamanada Ali amesema watuhumiwa
hao Jahmato Sabiro (20), Danana Dadebo (25) na Elias Chamuso (24) walikamatwa
juzi mchana saa 7.30 huko kijiji cha Kilomo kata ya Zinga Bagamoyo na
watakabidhiwa kwa Idara za Uhamiaji kwa taratibu zingine za kisherio
0 comments:
Post a Comment