WATU wanne wamekufa
papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa sehemu mbalimbali za miili baada ya
magari mawili tofauti waliokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso huko
Vigwaza Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani .
Tukio hilo limetokea
majira ya saa 12.30 jioni Julai 13 katika barabara kuu ya Dar esalaam Morogoro
na imehusisha gari T 610 Toyota Mark 11 ikiendeshwa na Venas Kimaro (44)
mfanyabiashara kuelekea Chalinze na gari ingine ni T 813 BZP Isuzu mini Bus
iliyokuwa ikitokea Chalinze.
Ajali hiyo inatajwa kuwa
ni miongoni mwa ajali mbaya za barabarani kutokana gari dogo kufinyangwa
mithili ya karatasi huku pia miili ya marehemu ikiharibika vibaya kwa
kukandamizwa na bodi ya gari hiyo.
Kaimu Kamanda wa
Polisi Mkoani Pwani Yusufu Ali amethibitisha tukio hilo ambapo alisema watu
wote wanne waliokufa walikuwa kwenye gari dogo na kwamba marehemu mmoja ndiye
katambulika ambaye ni dereva Kimaro na hadi asubuhi ya Julai 14 miili mingine
mitatu ilikuwa bado haijatambuliwa na ndugu na jamaa zao.
Kamanda Ali ambaye
pia ni Afisa upelelezi wa Polisi mkoani Pwani (RCO) amesema ajali hiyo ilitokea
baada ya kupasuka tairi la mbele hivyo kupoteza muelekeo na kugongana uso kwa
uso Isuzu hiyo na kusababisha vifo hivyo na majeruhi wanne kwenye basi hilo.
Amesema miili ya
marehemu wote ilipelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya Tumbi na majeruhi
wanne nao wanaendelea kutibiwa hapo hapo Tumbi na hali zao zinaendelea vema.
Kaimu Kamando huyo
ameongeza kuwa uchunguzi wa awali umeonyesha chanzo cha ajali hiyo ni mwendo
kasi wa dereva wa gari dogo hivyo kupelekea kupasuka tairi na kugongana uso kwa
uso na Isuzu.
0 comments:
Post a Comment