WATU wanne wamefariki
dunia na wengie saba kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti za barabarani
zilizotokea kwenye barabara kuu ya Dar esalaam Morogoro na Chalinze
Segera baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka na
jingine kugongana uso kwa uso Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Matukio hayo mawili ya
ajali yametokea usiku wa kuamkia Julai 25 kwa saa tofauti huku moja ikiwa
imetokea majira ya saa 5 usiku katika eneo la Vigwaza na ya pili saa 2.45 usiku
huo huo huko eneo la Mlima Wami.
Kamanda wa Polisi mkoani
humo Ulrich Matei amethibitisha ajali hiyo ambapo amesema katika ajali ya
Vigwaza watu wawili waliokufa ni Mohamed Athuman (32) dereva wa gari T
590 BXJ Toyota Coaster mini bus iliyokuwa ikitokea Morogoro kwenda Dar esalaam
na Hemed Mohamed (34) dereva wa gari T 102 CHW Mitsubishi Canter iliyokuwa
inatokea Dar esalaam Chalinze na miili hiyo imhifadhiwa hospitali ya
Rufaa ya Tumbi Kibaha.
Amewataja majeruhi wa
ajali hiyo ni Joseph Simbaya(50),mkazi wa Dar,Loitu Karangii(20),mkazi wa
Arusha ,William Saimairu(22)mkazi wa Arusha na Juma Shaban(22) mkazi wa Dar na
wote walimelezwa kwa matibabu katika hospitali ya Rufaa Tumbi na kwamba chanzo
cha ajali hiyo ni gari ya Canter kuhama njia na kugongana uso kwa uso na basi
hilo.
Katika ajali ingine
iliyotokea eneo la Mlima Wami Matei amesema ilisababisha vifo viwili na
majeruhi watatu na kwamba waliofariki ni Rajabu Ramadhan(25) na Jaribu
Yahaya(28) wote wakazi wa Changalikwa na waliojeruhiwa ni Masumbuko Mwatera
(31),Fred Mwasebo(24) mkazi wa Mbeya na Ally Kaziyabure.
0 comments:
Post a Comment