Home » » Askari kituo cha Osterbay wakamatwa na meno ya tembo 70

Askari kituo cha Osterbay wakamatwa na meno ya tembo 70

WATU tisa, wawili kati yao wakiwa ni askari wa Jeshi la Polisi kituo cha Ostabay jijini Dar esalaam wamekamatwa wilayani Kisarawe Mkoani Pwani kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha meno ya tembo (ndovu) 70 sawa na kilo 305 kinyume na sheria

Meno hayo ya tembo kwa mahesabu ya kawaida ni sawa na Tembo 35 ndiyo wameuawa na kwamba thamani ya meno hayo ni  zaidi ya sh, milioni 850 fedha za kitanzania.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao wamekamatwa saa 5.30 usiku wa Julai 28 huko Kisarawe na Askari Polisi na maliasili wilayani humo waliokuwa kwenye operesheni ya kukamata pembe za ndovu.

Matei amesema watuhumiwa hao walikamatwa katika kizuizi cha Kauzen kata ya Vikumbulu tarafa ya Chole ambapo walikuwa wakisafirisha meno hayo kwa kutumia gari T 357 ABK Toyota Surf kutoka wilayani humo kwenda jijini Dar esalaam

 Kamanda huyo wa Polisi Pwani amewataja watuhumiwa hao ni Hamidu  Hamadi wa Tandika Yombo, Musa Muhamed Ali wa Kinondoni Studio, Prospa Maleto mkazi wa Tandika hewa, Amir Bakar mkazi wa Mbagala Chalambe,Seif Mdumuka, Said Kadro na Ramadhan Athumani  wa Chanika.

Matei amewataja pia askari Polisi  wawili waliokamatwa pia kuwa ni Koplo Senga Idd Nyembo na PC Issa Mtama ambao wote wanadaiwa ni watumishi wa Jeshi la Polisi kituo cha Ostabay  jijini Dar esalaam na wanatarajiwa kutolewa Kisarawe walikokamatiwa na kufikishwa Kibaha makao makuu wa jeshi hilo mkoani Pwani kwa ajili ya hatua zingine za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Chanzo: tabianchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa