WATUMISHI wawili wa Halmashauri
ya mji Kibaha wamefukuzwa kazi mjini humo kwa tuhuma za kuhusika utovu wa
nidhamu kwa mwajiri,ubadhilifu na wizi wa fedha za miradi ya maendeleo zaidi ya
sh. milioni 15 ikiwemo ya ujenzi wa Zahanati na nyumba ya mganga wa afya.
Mbali ya watumishi hao wawili
kutimuliwa kabisa katika ajira zao, pia mtumishi mwingine mmoja naye kapewa
adhabu ya kukatwa asilimia 15 ya mshara wake kwa kipindi cha mwezi mmoja
kutoaka na utofu wa nidhamu kwa mwajiri wake.
Hatua hiyo imebarikiwa na Baraza
la madiwani wa halmashauri hiyo wakati wa kikao chake cha kawaida kilichoketi
leo Agosti mosi mjini humo.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo
Adhudadi Mkomambo aliwataja watumishi waliofukuzwa na kiasi cha fedha
walichokipora katika mabano ni Juma Sengoda afisa mtendaji ambapo anatuhumiwa
kuiba sh. milioni 14 kutoka katika akaunti ya fedha za ujenzi wa Zahanati ya
Garagaza.
Amesema mtendaji huyo alifanikiwa
kuchota kiasi hicho baada ya kufoji sahihi ya mwenyekiti huyo na muktasari wa
kutoa fedha za mradi huo benki.
Mkomambo alimtaja mtumishi wa
pili ni John Mwanga ambaye yeye anatuhumiwa kuiba kwa nyakati tofauti fedha za
ujenzi wa nyumba ya Mganga wa Zahanati ya Visiga sh.milion 1.5 benki kwa njia
hiyo hiyo ambapo licha ya kuanza kuchunguzwa hivi karibuni aliiba tena sh. laki
tatu 300,000 kwa njia hiyo ya kufoji sahihi na muktasari ya kutolea fedha benk.
Mkomambo aliwaeleza wajumbe hao
kuwa kutokana na utofu huo wa nidhamu na ubadhirifu wa fedha za miradi ya
wananchi watumishi hao hawana sababu tena ya kuendelea kuaminika kuwatumikia
wananchi mjini humo na hivyo mwajiri amewafukuza kazi.
Kufuatia hatua hiyo Mkurugenzi wa mji Kibaha Jenifa Omolo amethibisha watumishi hao wawili kupewa tayari barua za kuwaelekeza kuwa si waajiriwa tena wa halmashauri hiyo na kwamba alisisitiza hatua zaidi za kinidhamu zitaendelea kutolewa kwa watumishi ama mtu yeyote anayekiuka taratibu,kanuni na sheria za Utumishi wa Umma hivyo amewataka waajiriwa mjini humo kuchata kazi kiuadilifu ili kuleta tija kwa jamii.
0 comments:
Post a Comment