Home » » LEO NI LEO NGWASUMA NDANI YA KIBAHA

LEO NI LEO NGWASUMA NDANI YA KIBAHA

HATIMAYE lile onyesho la bendi ya FM Academia “Wazee wa Ngwasuma” mjini Kibaha limewadia na leo hii watajitupa ndani ya ukumbi wa Kontena huku lengo kuu likiwa ni kutambulisha nyimbo zao mpya.
Mwandaaji wa onyesho hilo, Othman Kazi, aliiambia Saluti5 kuwa hiyo ni nafasi adimu kwa wakazi wa Kibaha wa kushuhudia nyimbo mpya zitakazopatikana kwenye albam ijayo ya FM Academia.
FM Academia wanategemea kuzindua albam yao mpya “Chuki ya Nini” baadae mwaka huu na wamekuwa wakizitambulisha baadhi ya nyimbo zitakazounda albam hiyo katika kila pembe ya Tanzania.
Miongoni wa nyota wanaotegemewa kutamba katika onyesho la leo ni pamoja na rais wa bendi Nyoshi El Saadat, Pablo Masai, Patcho Mwamba na Malu Stoch na wengine kibao.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa