Home » » BREAKING NEWS: AMUUA MAMA YAKE KWA KUMPIGA MTALIMBO KICHWANI

BREAKING NEWS: AMUUA MAMA YAKE KWA KUMPIGA MTALIMBO KICHWANI

Habari zilizotufikia punde zinasema kuwa Kijana Fransis Chiza, mkazi wa Kiluvya A, Wilaya ya Kisarawe anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kumuua mamayake mzazi kwa kumpiga kwa mchi au mtalimbo kichwani na kufa papo hapo.
Inadaiwa kuwa kijana huyo ambaye ni motto wa pili wa mama huyo alifika jana usiku na kumgongea mlango mama yake lakini mamayeka hakuweza kumfungulia kutokana na kuwa na ulemavu jambo hilo lilimkasirisha na hivyo ilipofika asubuhi ya leo aliamua kutuliza hasira yake kwa kumpiga mama yake.

Baada ya kufanya tukio hilo kijana huyo alikimbia na baadaye kumkamata na wanakijiji. Jeshi la polisi wilaya ya kisarawe wameshafika eneo la tukio na kwa taarifa zaidi juu ya tukio hili zitakujia muda si mrefu….

Chanzo: Clouds FM

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa