Mwandishi wetu, Bagamoyo
Zaidi ya sh Milioni Mbili fedha za maendeleo ya kijiji
zinadaiwa kutumiwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Makombe Kata ya Lugoba
Wilaya ya Bagamoyo Hussein Mlwale na kusababisha wakazi wa eneo hilo kuamua
kumsimamisha uongozi .
Fedha hizo zinadaiwa zilitolewa na mwekezaji wa Kampuni ya TERRO
inayoshughulika na ubanguaji wa kokoto huko lugoba wilayani humo.
Sakata hilo limewekwa wazi na afisa Tarafa Mary Komba
mbele ya Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho Bw. Jeremiah Jerard na Ofisa Mtendaji
Kata ya Lugoba Athumani Mhami ambae alisema fedha hizo hazikufikishwa
kwenye uongozi huo.
Mary Komba amesema Mwenyekiti huyo ametafuna fedha
hizo ambazo zililenga kutumika kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo kwenye
kijiji hicho.
Hata hivyo baada ya kuvuja kwa hali hiyo mwenyekiti Mlwale anaedaiwa kutumia
fedha hizo milioni mbili za maendeleo ya kijiji amezisalimisha fedha hizo
polisi.
Sanjali na tuhuma hizo Mlwale analalamikiwa kutoitisha
mikutano ya mapato na matumizi ya kijiji na Wajumbe wa Halmashauri ya
kijiji hicho wamesimamishwa uongozi wakituhumiwa kutoweka wazi matumizi ya
fedha za marejesho zilizotolewa na wananchi baada ya kukopeshwa na serikali ya
kijiji hicho.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment