Na Mwandishi Wetu, Kibaha
MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, ameionea huruma
Hospitali ya Tumbi iliyoko Kibaha Mkoa wa Pwani, kwakukosa kifaa maalumu cha
kuhifadhia damu.
Amesema kuwa kukosekana kwa kifaa hicho katika hospitali hiyo, hakuwezi kukubalika badala yake zinatakiwa jitihada za haraka, ili kiweze kupatikana.
Mahiza aliyasema hayo jana Mjini Kibaha, alipokuwa akifungua rasmi ofisi za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mkoa wa Pwani kwa niaba ya ofisi nyingine tisa zilizoko katika mikoa tisa nchini.
“Mimi nashangaa sana, hii Hospitali ya Tumbi ni muhimu sana, hii siyo hospitali ya Mkoa wa Pwani peke yake, hii ni hospitali ya watu wote kwa sababu, inahudumia mamia ya watu.
“Pamoja na umuhimu huu, Hospitali ya Tumbi haina kifaa cha kuhifadhia damu, yaani utashangaa mtu akipata ajali kule Mbwewe au Chalinze, akifikishwa Tumbi damu ya kumwekea lazima eti itoke Amana au Muhimbili Dar es Salaam.
“Hii ni akili gani, yaani sisi tumesoma mpaka milango ikafunguka na kujifunga, lakini hatuoni umuhimu wa kuwa na kifaa cha kutunzia damu mpaka tusubiri damu itoke Dar es Salaam, hii akili gani?
“Haiwezekani, hiki kifaa lazima kiwepo hapa, kama hakuna fedha basi tumieni fedha za dharura, ili mhakikishe kifaa hiki kinakuwapo hapa kwa sababu hospitali hii ni muhimu sana, kama ni mahitaji ya vifaa vingine, subirini kwanza ili mnunue hiki,” alisema Mahiza.
Kuhusu majukumu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, alisema Watanzania wanatakiwa kujiunga na mfuko huo, kwa kuwa ni muhimu kuliko fedha wanazoweka benki.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emmanuel Humba, alisema kufunguliwa kwa ofisi ya mfuko huo katika Mkoa wa Pwani ni mwendelezo wa mfuko huo kuzidi kujitanua kwa lengo la kutoa huduma kwa wananchi wengi zaidi.
Alisema kwamba, pamoja na kwamba Bima ya Afya imekuwa ikipata wateja wengi zaidi, bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali, zikiwamo wananchi kutoelewa umuhimu wa mfuko huo na ukosefu wa dawa.

Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment