Julieth Ngarabali, Pwani
RAIS mstaafu awamu ya pili katika Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaji Ally Hassan Mwinyi amekemea tabia ya baadhi ya akina dada na akina mama nchini kukataa kunyonyesha watoto wao kwa kutumia matiti yao kwa kuhofia kuanguka ama kuwa makubwa.
Mwinyi amekemea tabia hiyo kwenye Msikiti wa Masjid Quba mjini Kibaha wakati akihitimisha mafunzo ya mwezi mmoja kwa wanawake 150 wakiislamu yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kujitambua katika maisha yao.
“Siku hizi imekwa ni fasheni kwenye maeneo mengi nchini kukuta akina mama ama wadada wakishajifungua tu hukataa kunyonyesha ama hunyonyesha siku kadhaa na kisha kumuachisha ziwa mtoto kwa kuhofia matiti kuanguka ama kuwa makubwa” alisema Mzee Mwinyi
Rais huyo mstaafu awamu ya pili amesema si jambo la busara hata kidogo la kutowanyonyesha watoto wao na kwamba ni kuwanyima haki yao ya msingi na kuwakoseha kinga ya mwili.
Kwa upande mwingine Mwinyi amekemea tabia ya wazazi kuwapa watoto wao majina yasiyo na maana ama tafsiri njema katika makuzi mfano ikudhani, Tabu, Shida na hivyo kushauri watoto wapewe majina mazuri yenye kuleta maana na Baraka katika maisha yao.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment