Home » » MANYASI NAHODHA MPYA JKT RUVU

MANYASI NAHODHA MPYA JKT RUVU

na Clescencia Tryphone
BENCHI la ufundi la klabu ya Maafande wa JKT Ruvu limemkabidhi unahodha mshambuliaji mkongwe Sostenes Manyasi, akirithi mikoba iliyokuwa ikishikiliwa na beki, Shaibu Nayopa.
Kocha Mkuu wa JKT Ruvu, Charles Kilinda, aliliambia Tanzania Daima jana kuwa, Nayopa amehamishiwa kikazi mkoani Kigoma, hivyo kufanya shughuli nyingine nje ya soka.
Kilinda alisema, nahodha huyo mpya, Manyasi atasaidiana na Hussein Bunu pamoja na George Minja na kuwa, kuondoka kwa Nayopa hakujaacha pengo katika timu yake, kwa kuwa ana mbadala wa kuziba pengo hilo.
Alisema timu yake inaendelea na mazoezi na mechi za kirafiki na kuelezea kufurahishwa na ligi kusogezwa ili aweze kupata mechi tatu za kirafiki kabla ya Septemba 15.
Aliongeza kuwa miongoni mwa mechi hizo tatu, anatarajia kucheza moja na Yanga na nyingine African Lyon, huku timu ya tatu bado anatazama timu.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa