Na Antony Siame, Bagamoyo
SHIRIKA la Hope Foundation Club kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mji mdogo wa Bagamoyo, wamezindua kampeni ya kuufanyia usafi mji huo.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo mjini hapa mwishoni mwa wiki, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo, Princess Marsland, alisema wamedhamiria kuuweka safi mji huo kutokana na historia iliyopo Bagamoyo.
Alisema wageni wengi wanatembelea mji huo kuangalia na kupata historia ya mambo ya kale yaliyopo hapo.
Alisema atahakikisha elimu inatolewa kwa kila mkazi na hatimaye usafi uanzie nyumba kwa nyumba ndipo waendelee mitaani na barabara zote zinazozunguka mji huo.
Alisema katika kampeni hiyo watashirikiana na wadau wengine kuhakikisha mji unakuwa katika hali ya usafi akifananisha na mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
Alisema haipaswi mji wa kitalii unaotembelewa na watu kutoka mataifa mbalimbali, ukawa mchafu na kusababisha sifa mbaya.
Wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo waliwashirikisha watoto zaidi ya 50 wanaohudumiwa na Shirika hilo na miongoni mwao wakiwa yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.
Naye, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji mdogo wa Bagamoyo, Musa Athumani, alisema wamejipanga kuweka mji huo safi na ndiyo maana wameamua kushirikisha wadau mbalimbali katika kampeni hiyo.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment