Home » » KOKA ATOA MILIONI MBILI KUCHANGIA UJENZI WA MADARASA YALIYOUNGU ASHULE YA MSINGI KONGOWE

KOKA ATOA MILIONI MBILI KUCHANGIA UJENZI WA MADARASA YALIYOUNGU ASHULE YA MSINGI KONGOWE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

MBUNGE wa jimbo la Kibaha Mjini, Silvestry Koka, ametoa kiasi cha shilingi milioni mbili zitakazosaidia kutumika kuezeka madarasa yaliyojengwa baada ya kuungua katika shule ya msingi Kongowe.

Mwaka 2016 vyumba vitatu vya madarasa na ofisi, shuleni hapo viliungua kutokana na kutokea shoti ya umeme .

Koka alitoa mchango huo, wakati alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara ,Miembesaba 'A'kata ya Kongowe katika muendelezo wa ziara yake ya jimbo.

Aliomba fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo pamoja na kukamilisha ujenzi wa shule hiyo zisimamiwe na kutumika kwa matumizi lengwa.

Akizungumzia changamoto za kielimu kijumla ,alisema kwasasa maeneo mengi yanakabiliwa na tatizo la upungufu na uchakavu wa miundombinu .
Koka aliitaka jamii ,wadau ,kamati za shule na viongozi mbalimbali kushiririkiana kuongeza vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo mashuleni .

"Kulikuwa na kero kubwa ya uhaba wa madawati na kusababisha watoto wetu kusoma huku wakiwa wamekaa chini na kupata vifua kutokana na vumbi""Lakini tumejitahidi tumemaliza kero hiyo ,kilichobaki kwasasa ni tatizo la miundombinu,ambapo tushikamane kumaliza ama kulipunguza ili watoto waondokane na mlundikano wa kusoma kwenye darasa moja ama kusoma kwa awamu" alifafanua Koka.

Koka aliwaasa wazazi na walezi ambao watoto wao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza na darasa la kwanza kuwapeleka shule .Alisema elimu ndio nguzo na hazina ya watoto ,hivyo ni jukumu la wazazi kuona umuhimu wa kuwapa haki hiyo watoto hao.

Kuhusu tatizo la kutumia maji ya visima badala ya maji safi na salama kutoka Dawasco huko eneo la Ngungwa kata ya Kongowe ,alisema linashughulikiwa .Alisema tatizo la maji lililokuwepo awali Kibaha ,sivyo ilivyo sasa kwani wamepiga hatua ,mradi wa Ruvu Juu na Ruvu Chini imekamilika hivyo kazi iliyobakia ni kusambaza .

Katika afya ,Koka alielezea anaendelea kusimamia changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo uhaba wa watumishi,vifaa tiba na madawa.
Alisema kutokana na hilo ,mwezi June mwaka jana ,alileta kontena la vifaa tiba mbalimbali lililogharimu mil.400 na vifaa hivyo vilisambazwa kituo cha afya mkoani na zahanati zilizopo jimboni hapo. 

Alieleza ataendelea kusimamia asilimia 10 ya vijana ,wazee,wanawake,walemavu kwenye mapato ya ndani ya halmashauri ya Mji wa Kibaha ,ili inufaishe makundi hayo.Koka alisema kwasasa ,asilimia 10 inatakiwa igawanywe asilimia 4 akinamama,asilimia 4 vijana,wazee na walemavu asilimia moja ,moja.

Nae afisa elimu kata ya Kongowe,Aziza Matekenya alisema wakati baadhi ya majengo ya shule ya msingi Kongowe yakiungua shule hiyo ilikuwa na wanafunzi 1,840.Alisema halmashauri ilitoa milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa hayo na imeahidi kuongeza milioni 20 kwa ajili ya umaliziaji.

Aziza alieleza,kwasasa shule ina jumla ya vyumba 12 vya madarasa vinavyotumika ,vitatu vichakavu ambapo inahitaji vyumba vya madarasa 40 ili kukidhi mahitaji.Shule hiyo ilijengwa miaka ya 70 ,kwasasa ina wanafunzi 2,820 na walimu 35

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa