Mwanamitindo
wa Kimataifa afanyae kazi zake nchini Marekani, Flaviana Matata (wa
tatu kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo alilojenga la
madarasa mawili na ofisi ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi kwa shule ya
msingi Msinune, iliyopo kata ya Kiwangwa wilayani Bagamoyo Mkoa wa
Pwani jana.
Mwanamitindo
wa Kimataifa afanyae kazi zake nchini Marekani, Flaviana Matata kushoto
akikabidhi mipira kwa wanaafunzi wa shule hiyo, Flaviana ni mlezi wa
shule hiyo.
Mwanamitindo
Flaviana akionesha cheti cha heshima alichotunukiwa na uongozi wa kata
ya Chiwangwa baada ya kuwajengea majengo ya shule.
Flaviana
akipokea zawadi ya mbuzi kutokea kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Msinune,
Ramadhan Mtokeni (kushoto) huku Diwana wa kata ya Chiwangwa (kulia)
Malota Kwagga na Afisa elimu wa kata hiyo Blasius Alphonce kulia kwa
diwani na Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Msinune, Alex Lugaigalila
wakiangalia.
Flaviana akiwahoji wanafunzi hao maendeleo yao ya masomo shuleni hapo.
Flaviana
akiwa amekalia moja kati madawati 45 ambayo aliyatoa kwa shule hiyo
mwaka jana, kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Msinune, Alex
Lugaigalila na kushoto ni Afisa elimu wa kata hiyo Blasius Alphonce.
Flaviana akipokea cheti cha heshima kutokea kwa Mtendaji wa Kijiji cha Msinune, Memory Mbangwa cha kutambua mchango wake huo.
Flaviana akiwa na watendaji wa kijiji hicho na kata pamoja na wanakijiji waliojitokeza siku hiyo.
Alipata wasaha wa kupiga picha na wanafunzi pia siku hiyo ambao walimpongeza kwa msaada wake huo
Na Evance Ng’ingo
MWANAMITINDO
wa kimataifa afanyaye shughuli zake nchini Marekani, Flaviana Matata
madarasa mawili ya shule za msingi iliyopo katika kijiji cha Msinune
kilichopo kata ya Kiwangwa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Flaviana
alipewa jukumu la ulezi wa shule hiyo na wanakijiji wa Msinune mwaka
2014 wakati alipoenda kuwasaidia wanafunzi mabegi ya shule, walimpatia
jukumu la kuwatengenezea vyoo, ofisi na nyumba za walimu pamoja na
kumalizia ujenzi wa darasa.
Tangia
alipopewa majukumu hayo alianza kwa ujenzi wa vyoo vya walimu na
wanafunzi, na juzi alienda kukabidhi jengo la madarasa, darasa la saba
na la sita pamoja na ofisi ya Mkuu wa Shule.Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo Flaviana alisema, tangia alipopewa jukumu
la ulezi wa shule hiyo amekuwa akihangaika huku na kule kupata fedha za
kutatua kero za shule hiyo.
Alisema,
kwa kufanikiwa kukabidhi jengo hio la madarasa anaona kuwa ameshiriki
kikamilifu katika kutekeleza jukumu lake kama mwanajamii la kusaidia
maendeleo ya elimu kwa jamii iliyokuwa na uhitaji mkubwa.
Alisema”
sisi kama vijana kama watanzania tunalo jukumu la kujitokeza na
kusaidia maendeleo ya elimu na sekta nyingine muhimu nchini kwa kuwa
hili sio jukumu la serikali peke yake, sasa nimeshatengeneza vyoo vya
walimu na wanafunzi na leo nakabidhi darasa”
Kwa
upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Alex Lugaigalila alisema ujenzi
wa darasa huo utawaongezea ufanisi wanafunzi katika masomo yao huku
akibainisha wazi ushiriki wa Flaviana kwenye maendeleo ya shule hiyo
umeongeza hamasa ya wanafunzi kusoma.
Kwa
upande wake Afisa wa elimu wa Kata hiyo,Blasius Alphonce alisema kwa
ujenzi wa jengo hilo, Flaviana amesaidia jitihada za serikali katika
kuendeleza elimu kwenye kata hiyo yenye vijiji vitano.
Jengo
hilo la darasa lililojengwa lina vyumba viwili vikubwa vilivyoezekwa kwa
bati huku likuwa na madirisha makubwa yanayowezesha kupitisha hewa na
chumba cha mwalimu mkuu.
0 comments:
Post a Comment