Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama akizungumza na wakazi waliovamia eneo la hifadhi ya msitu wa Dutumi mara baada ya kukagua msitu huo na kukuta uharibifu mkubwa ndani ya Msitu huo.
Mkuu wa Wilaya Assumpter akimshika mtoto mmoja wapo anayeishi na wazazi wake kwenye kambi ya watu wanaokata misitu na kuchoma mkaa , hapo alikuwa akiwauliza wazazi hao kuwa hawawatendei haki watoto wao kwani ndani ya kambi hizo hakuna mahitaji muhimu kama hispitali, shule, maji safi pamoja na malazi yenye hadhi ya kuishi binaadamu
Sehemu ya msitu wa Dutumi ambao umefyekwa miti yote mikubwa na wananchi waliovamia msitu huo
Mkuu
wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama ametoa mwezi mmoja kwa wavamizi
wa eneo la hifadhi ya msitu wa Dutumi kuondoka mara moja ifikapo Oktoba 4
mwaka huu.
DC
Assumpter amesema hayo baada ya kwenda kuutembelea msitu huo eneo la
Tengefu la hifadhi lililopo katika Mkoa wa Pwani baada ya kupata taarifa
kuwa kuna watu ambao wamevamia na wameweka makazi katika eneo hilo
isivyo rasmi.
0 comments:
Post a Comment