Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Makamu
wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi akifungua mkutano wa Jumuiya ya
Maendeleo ya Mkoa Kaskazini Unguja katika Ukumbi wa Baraza la
Wawakilishi la zamani Kikwajuni.
Mjumbe
wa Kamati ya Uongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Mkoa Kaskazini Unguja
Ayoub Mohammed Mahmoud akieleza mafanikio ya Jumuiya tokea ilipoasisiwa
mwaka jana katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la
zamani Kikwajuni.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Mkoa Kaskazini
Unguja Ali Juma Ali akiwaeleza wananchama wa Jumuiya hiyo mikakati na
mipango ya kuiendeleza ili kufikia malengo yake katika mkutano
uliofanyika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni.
aadhi
ya wajumbe wa mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Mkoa Kaskazini Unguja
wakifuatilia mkutano huo uliofanyika Baraza l a Wawakilishi la zamani
Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Maendeleo ya Mkoa Kaskazini Unguja Ali Juma Ali akiagana
na Makamu wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi baada ya mkutano wa
Jumuiya hiyo uliofanyika Ukumbi wa Baraza la wawakilishi la zamani
Kikwajuni.Picha na Makame Mshenga.
Na Miza Kona, MAELEZO .
MAKAMU
wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, ameitaka Jumuiya ya Maendeleo ya
Mkoa wa Kaskazini Unguja kuzidisha mshikamano ili kuweza kubadilika
kielimu na kuleta maendeleo mazuri mkoani humo.
Balozi
Seif ameyasema hayo katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi
Kikwajuni mjini Zanzibar katika mkutano wa Jumuiya hiyo.
Alisema vijana wengi wa mkoa huo wanakosa kuingia katika ushindani wa soko la ajira kutokana na kukosa sifa zinazohitajika.
Balozi
Seif alisema jumuiya inaweza kuleta mafanikio makubwa kwa kushirikana
pamoja na kuzidisha mshikamano katika dhamira ya kuibadilisha jamii ya
mkoa huo kielimu.Alifahamisha
kuwa elimu ndio silaha pekee inayoweza kuwakomboa vijana na kuwawezesha
kukubalika katika ajira mbalimbali na hivyo kuondokana na umasikini.
“Ni
wakati sasa wa kubadilika kwa kuwekeza katika elimu ya watoto wetu ili
kuwainua vijana na kuwawezesha kuhimili ushindani kwa kuwa na sifa
zitakazoweza kuajiriwa au kujiajiri,” alifahamisha Balozi Seif.
Alieleza
vijana wengi wa mkoa huo hawana mwamko wa kusoma, jambo linachangia
mkoa wa Kaskazini kuwa nyuma kielimu na kimaendeleo ikilinganishwa na
mikoa mingine nchini.
Amehimiza
kuwepo ushirikiano wa pamoja baina ya viongozi na wana jumuiya katika
kuishajiisha jamii ili iweze kubadilika kiuchumi na kuacha kuingiza
itikadi za siasa katika suala la kuleta maendeleo.
Balozi Seif alisema jumuiya ina nia ya kuimarisha umoja na kuleta maendeleo katika mkoa huo.
Aidha
Makamu wa Pili wa Rais amewasisitiza viongozi wa majimbo na serikali
katika mkoa huo kudumisha ushirikiano na kuwasaidia vijana wasio na
uwezo wa kujikimu kwa kuwapa msukumo wa kimaendeleo pamoja na
kuishajiisha jamii kujiunga jumuiya hiyo.
Jumuiya
Maendeleo ya Mkoa wa Kaskazini Unguja (NUDO), imeasisiwa mwezi Aprili
2016, na sasa ina zaidi ya wanachama zaidi ya 1000.
Lengo
la kuanzishwa kwake ni kuendeleza, kuwezesha na kuijengea uwezo jamii
ya mkoa huo katika kuinua ustawi wake kiuchumi, kijamii na mazingira.
0 comments:
Post a Comment