Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe Hamisi Dikupatile na Mganga Mkuu wa wilaya Elizabeth na viongozi wengine katika ukaguzi wa kituo cha Afya Maneromango.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya kisarawe katika ukaguzi wa utoaji huduma za afya kwenye Kituo cha Afya Maneromango.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wataalam wa Afya na wagonjwa katika kituo cha Afya Maneromango.
Baadhi ya wagonjwa wakisubiri kupata huduma za afya katika kituo cha Afya Maneromango.
WATAALAM
wa afya katika kituo cha Maneromango kilichopo wilaya ya Kisarawe
Mkoani Pwani wamefurahishwa kwa juhudi ya serikali ya awamu ya tano ya
kuweka mkakati wa kukarabati kituo chao cha Afya.
Furaha
ya wataalam hao wa Afya ilijitokeza wakati wa ziara za kikazi za Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipotembelea
kituoni hapo kukagua maendeleo ya utoaji wa huduma za afya.
Wataalam
hao wamesema kwasasa wanafanya kazi katika mazingira magumu kutokana na
changamoto kubwa ya miundombinu.Kituo hicho kwasasa hakina chumba cha
upasuaji, wodi za wagonjwa sambamba na ukosefu wa jengo Maalum la
maabara.Kutokana na hali hiyo, Serikali imeamua kuwasaidia wananchi wa
maeneo hayo kwa kuwajengea miundombinu ya jengo la upasuaji, maabara,
nyumba ya watumishi.
Pia
ujenzi wa miundombinu mingine unafanywa kwa fedha za ufadhili kutoka
serikali ya Canada na tayari serikali inatarajia kupeleka Sh.milioni 500
kuanza ujenzi wa miundombinu hiyo.
Akizungumza
na wataalam hao, Naibu waziri jafo amebainisha kwamba changamoto ya
miundombinu ya afya imekuwa kubwa ndio maana serikali imeamua kuanza
kufanya ujenzi wa vyumba vya upasuaji na uimarishaji wa vituo vya afya
zaidi ya 150 hapa nchini ili kupunguza vifo vya mama wajawazito na
watoto.
Jafo
amewaambia wataalam na wagonjwa waliokuwepo kituoni hapo kwamba
serikali ya awamu ya tano imejipanga kuimarisha sekta ya afya hapa
nchini.
0 comments:
Post a Comment