Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (katikati) akiwasili
katika kiwanda cha kuunganisha Matrekta ya URSUS-TAMCO, kilichoko Kibaha
mkoani Pwani kuangalia kazi ya uunganishaji matrekta zaidi ya 200
pamoja na kusikiliza changamoto zinazoukabili mradi huo.
Na. Benny Mwaipaja-Kibaha
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango akiwasha moja ya matrekta
yaliyounganishwa katika Mradi wa Kuunganisa Matrekta ya URSUS-TAMCO,
uliopo katika eneo la Kibaha mkoani Pwani, alipotembelea mradi huo.
Meneja
Mradi wa Kuunganisha Matrekta ya URSUS, Kibaha mkoani Pwani, Mhandisi
Adam Mbura, akimweleza Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor
Mpango, moja ya majembe yaliyounganishwa kupitia mradi huo.
Mafundi
pekee wa kike katika Mradi wa Kuunganisha Matrekta ya URSUS katika eneo
la Kibaha Mkoani Pwani, Bi. Fatma Abbass (kulia) na Rahabu Japhet
wakisikiliza wosia na maelekezo kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango,
Dkt. Philip Isdor Mpango, (hayupo pichani) alipotembelea Mradi huo.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (aliyevaa tai) akiwa
katika picha ya pamoja na vijana mafundi wanaounganisha matrekta katika
Mradi wa kuunganisha Matrekta ya URSUS, kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.
Benny Mwaipaja, (kushoto) akizungumza na Meneja Mradi wa kuunganisha
Matrekta ya URSUS, Mhandisi Adam Mbura, (katikati) katika eneo la mradi
huo uliopo Kibaha mkoani Pwani ambapo tayari matrekta 204 yameunganishwa
katika awamu ya kwanza ya mradi huo ambapo zaidi ya matrekta 2,400 na
zana zake yanatarajiwa kuunganishwa, wakati Waziri wa Fedha na Mipango,
Dkt. Philip Mpango alipofanya ziara kwenye mradi huo.
Sehemu ya matrekta 204 yaliyounganishwa katika Mradi wa Kuunganisha Matrekta ya URSUS-TAMCO, katika eneo la Kibaha mkoani Pwani
WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ametembelea mradi wa
kuunganisha matrekta ya Ursus, uliopo Kibaha mkoani Pwani na kusisitiza
kuwa Serikali imedhamiria kuendeleza kilimo nchini ili kukuza sekta ya
viwanda.
Tayari
Matrekta 204 yenye uwezo wa HorsePower 50 yamekwisha unganishwa
yakisubiri kuuzwa kwa watumiaji hatua ambayo Dkt. Mpango amesema
itaongeza tija katika kilimo na kukuza ajira hususan kwa kundi kubwa la
vijana.
Ameahidi
pia kuwa Serikali itayafanyiakazi haraka maombi ya Shirika la Maendeleo
la Taifa NDC la kutaka kupata kibali cha kuajiri zaidi ya wafanyakazi
90 watakaohusika na mradi huo pamoja na kutoa shehena ya Matrekta 267
yaliyokwama katika Bandari ya Dar es Salaam ili yaweze kuuzwa kwa
wananchi kuendeleza kilimo.
Kwa
upande wake, Meneja wa Mradi huo kutoka Shirika la Maendeleo la
Taifa-NDC, Mhandisi Adam Mbura, amesema mradi huo utahusisha pia
uanzishwaji wa vituo vinane katika kanda mbalimbali kwa ajili kuuza
matrekta, zana na vifaa vingine pamoja na kutoa huduma kwa wateja.
Amesema
kuwa kukwamuliwa kwa makontena 64 yaliyokwama bandarini yakiwa na
matrekta hayo 267 pamoja na vipuri vya kuunganisha Matrekta hayo pamoja
na baadhi yaliyopo katika eneo la Mradi la TAMCO, Kibaha mkoani Pwani,
kutawezesha kukamilisha haraka kwa kazi hiyo.
Baadhi
ya vijana wanaofanyakazi katika mradi huo wamesema kuwa wamenufaika na
ujuzi wanaoupata kutoka kwa wataalamu wa ufundi kutoka nchini Poland na
kuahidi kuuendeleza ujuzi huo kwa vijana wenzao ili mradi huo uweze kuwa
na manfaa kwa kutatua changamoto mbalimbali za kiufunsi zitakazokuwa
zikiwakabili wakulima
Mradi
wa kuunganisha Matrekta ya URSUS-TAMCO, Kibaha Mkoani Pwani
unafadhiliwa na Serikali ya Poland ambapo kiwanda kikubwa cha
kuunganisha matrekta kinatarajiwa kujengwa katika eneo hilo na yatauzwa
kwa gharama nafuu, kati ya shilingi milioni 38 hadi milioni 42 kulingana
na ukubwa na uwezo wa trekta.
0 comments:
Post a Comment