Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
.Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga akizungumza na wananchi wa vijiji vinne ambavyo vina mgogoro wa ardhi katika mkutano uliofanyika Mwanambaya .
Mbunge wa jimbo la Mkuranga , Abdalah Ulega akizungumza na wapiga kura wake juu ya mgogoro wa shamba lenye ekari 90 katika kijiji cha Mkuranga.
.Sehemu ya wananchi wakimsikiza mkuu wa wilaya juu ya mgogoro unao wakabili
Mkuu
wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga ameagiza shughuli zote za upimaji
wa ardhi kusimama kwa sasa mpaka watakapotoa kibali cha upimaji.
Mkuu
Wilaya alitoa agizo katika mkutano na wananchi wa wilaya kuhusiana
na mgogoro wa ardhi, ambapo vijiji vinne vinavyodaiwa kuvamia shamba la
familia ya Rajwani mwenye asili ya kihindi lenye ukubwa wa ekari 2472.
Vijiji hivyo vinne ni Mwambaya,Lunzando,Mipeko na mlamleni vilivyopo kwenye Kata ya mipeko na Tambani.
Sanga
amesema kuwa kwa sasa hakuna mtu kutoka Halmashauri wala maafisa
mipango miji kupima ardhi mpaka awe na kibali kutoka wilayani na
kuongeza kuwa Madiwani na Wenyeviti wa vitongoji kutoruhusu mtu kupima
ardhi mpaka awaoneshe kibali kutoka wilayani.
Aidha
amewataka wananchi wa vijiji hivyo kifanya kazi zao kwa Uhuru bila hofu
yeyote kwani wilaya hiyo ipo salama."tumejipanga vizuri Mimi mwenyewe
ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na wahakikisheni mupo
salama,msiache kwenda mashambani,msiache mazao shambani kavuneni mazao
yenu hakina wakuwabigudhi.alisema Sanga.
Wakati
huohuo ametoa wito kwa madereva wabodaboda wilayani humo wametakiwa
kuvaa kofia ngumu pindi wanapoendesha pikipiki na kuacha kupakia watu
wawili kwa pikipiki moja ‘Mishakaki’.
Naye
Mbunge wa jimbo la mkuranga Abdalah Ulega amewatoa hofu wananchi hao
kwa kuwa suala lao linashughulikiwa na wamempa notisi ya siku 90 ya
kujieleza kuhusiana na eneo hilo.
Ulega
aliwaahidi wananchi hao kuwachangia kiasi cha shilingi milioni moja
kama sehemu ya mchango wake katika kusaidia kutatua tatizo hilo.
0 comments:
Post a Comment