Home » » KITUO CHA AFYA CHALINZE CHAANZA KUFAWANYIA OPARESHENI WAGONJWA

KITUO CHA AFYA CHALINZE CHAANZA KUFAWANYIA OPARESHENI WAGONJWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Omary Mngindo, Lugoba

KITUO cha afya cha Chalinze kilichopo Kitongoji cha Bwilingu halmashauri ya Chalinze Bagamoyo Mkoa wa Pwani kimeanza kuwafanyia operesheni wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo kituoni hapo.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mwanasheria Ridhiwani Kikwete ndiye aliyechokonoa hoja hiyo alipomtaka Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo kumpatia uhakika wa jambo hilo ambalo analisikia kwa watu kwamba Kituo hicho kimeshaanza zoezi la kuwafanyia upasuaji wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo.

"Nimesikia maneno kutoka kwa wakazi wakisema kwamba Kituo chetu cha afya Chalinze kimeshaanza kuwafanyia upasuaji wagonjwa wanaokwenda kwa ajili ya huduma hiyo, Mganga Mkuu tunaomba ulitaarifu Baraza hili taarifa hizo zilizo njema zina ukweli gani?," aliuliza Ridhiwani.

Akijibu swali hilo, Dr. Isaack Makungu aliwathibitishia Madiwani hao kwamba taarifa hizo zina ukweli na tayari akina mama 10 wajawazito wameshapatiwa huduma ya upasuaji kisha kupata watoto wakiwa salama na afya njema pamoja na wazazi wenyewe wakiwa na afya iliyo njema.

"Ni kweli Kituo chetu kimeshaanza kazi ya kuwafanyia upasuaji akina mama wajawazito ambao wamebainika hawana uwezo wa kusukuma mtoto ambapo watu kumi tumeshawapatia huduma hiyo wakiwa salama wao pamlja na watoto wao," alisema Dr. Makungu.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Said Zikatimu aliliambia Baraza hilo kwamba hatua hiyo ni faraja kwao kwani itasaidia mambo mengi kwanza kuwapunguzia saafari ndefu ya kwenda Tumbi, Bagamoyo au Muhimbili, poa mafuta ambayo yalikuwa yanatumika kusafirisha wagonjwa kweda maeneo nayo.

"Taarifa hiyo ni faraja kwetu kwani itasaidia wagonjwa ambao awali walikuwa wanasafirishwa kwenda Tumbi, Bagamoyo au Muhimbili, lakini tunatakiwa kujenga uzio kutoka chumba cha upasuaji kwenda wodini ili mgonjwa anapotoka kufanyiwa upauaji asiwe anaonekana na watu wengine," alisema Zikatimu.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa