Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Diwani wa Kata hiyo, Ramadhani Mkufya (CCM), aliibua hoja hiyo katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika juzi mjini Lugoba, ambapo alisema wajawazito na wagonjwa wengine katika kata yake wamekuwa wakikabiliwa na adha hiyo kwa muda mrefu.
Kutokana na hali hiyo, Mkufya aliiomba Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kupitia Mkurugenzi Mtendaji wake, Edes Lukoa, kuhakikisha inapeleka gari la wagonjwa katika kata hiyo ili kuweza kuokoa maisha ya wananchi wake hususani wajawazito.
“Kibindu hakuna gari la wagonjwa badala yake wagonjwa wakiwemo wajawazito wamekuwa wakipanda magari yanayobeba mkaa kwa ajili ya kufuata huduma ya afya sehemu mbalimbali, hivyo naiomba Halmashauri isaidie kutatua jambo hili kwa haraka,” alisema Mkufya.
Alisema kama halmashauri haina uwezo wa kununua magari mapya, ni vyema kwa sasa wakaweka jitihada za kutengeneza magari mabovu yaliyopo katika Halmashauri hiyo ili yaweze kuwasaidia wananchi hao wakati taratibu za kununua magari mapya zikiendelea kufanyika.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Edes Lukoa, alisema kilio cha diwani huyo ni sahihi na kwamba halmashauri itatumia mapato yake ya ndani katika kumaliza tatizo hilo.
Alisema halmashauri inatengeneza ambulance moja mbovu iliyokuwa ikifanya kazi katika maeneo ya Kwamrohombo na kwamba inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu na itapelekwa katika Kata hiyo.
Alisema Kata ya Kibindu inahitaji gari la wagonjwa, kwa sababu wajawazito 30 hujifungua ndani ya mwezi mmoja.
Chanzo:Mtanzania
0 comments:
Post a Comment