Imeandikwa na John Gagarini, Kibaha
JESHI la Polisi mkoani Pwani linawashikilia Makamba Sixbert (32) na
Doto Mwinyi (45) wakazi wa Mlingotini wilayani Bagamoyo, kwa tuhuma za
kukutwa na zana za uvuvi haramu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Kibaha
na Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Jonathan Shana, watu hao walikamatwa
kwenye msako.
Shana alisema watuhumiwa Sixbert na Mwinyi walikamatwa Julai 25
majira ya saa 8:00 usiku maeneo ya Mlingotini kata ya Zinga baada ya
msako maalumu wa makosa mbalimbali ukihusisha askari wa Jeshi la polisi
wilaya ya Bagamoyo, Polisi Makao makuu, Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ) na maofisa uvuvi na mifugo wa wilaya hiyo.
0 comments:
Post a Comment