Home » » WAZIRI LUKUVI AKESHA AKISHUGHULIKIA MIGOGORO YA ARDHI.

WAZIRI LUKUVI AKESHA AKISHUGHULIKIA MIGOGORO YA ARDHI.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ajikuta akikesha ofisini kwake pamoja na wananchi takriban 189 wenye Matatizo na Kero za ardhi.

Mhe. Waziri ametumia takriban saa 20 kusikiliza kero za wananchi ambao waligoma kuondoka ofisini kwake hadi kero zao zitakapopatiwa ufumbuzi. Kazi hiyo ilianza  majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 9 usiku.
Hata hivyo wananchi walilazimika kulala Wizarani wakisubiri kuonana na Waziri kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya wananchi hao.

Wananachi wengi wenye matatizo na Kero za ardhi kutoka maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Mkuranga, Kibiti na Dar es salaam kwa ujumla wametumia fursa hii ya kipekee ya kuonana na Waziri mwenye dhamana ya Ardhi na kumuelezea kero zao na hatimaye kupatiwa ufumbuzi papo hapo.

Wananchi hao wamesifu hatua hii ya Waziri Lukuvi kukutana nao ana kwa ana na kuzitatua kero zao za ardhi kwa kuwa haijawahi kutokea. Nae Bwana Francis Kamara mkazi wa Ilala jijini Dar es salaam amemuomba Waziri aweze kuwaajibisha watumishi ambao wanakwamisha jitihada zake hadi kupelekea yeye kukutana na wananchi moja kwa moja.

Mwanzoni mwa mwezi Juni 2017 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi alitoa Tangazo la kuwataka wakazi wa kanda ya Dar es Salaam na Pwani ambao wangependa kumuona,  wafike katika ofisi yake ya kanda ya Dar es Salaam iliyopo ghorofa ya pili, jengo la Wizara ya Ardhi – Magogoni, Kivukoni ili kujiandikisha majina yao, anuani na namba zao za simu.

Aidha, Mhe. Waziri atafanya ziara kama hii katika kanda nyingine mara baada ya kukamilisha zoezi hilo katika Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa