POLISI mkoani Pwani inaendelea kumtafuta mwanafunzi wa shule ya
sekondari ya Rafsanjani iliyopo Soga tarafa ya Mlandizi wilayani Kibaha
mkoani Pwani baada ya kuchoma bweni la wasichana la shule hiyo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Bonaventura Mushongi,
mwanafunzi huyo ambaye hakuweza kufahamika alichoma bweni liitwalo Umoja
juzi saa 4:00 usiku.
Alisema hata hivyo, tukio hilo halikuwa na madhara kwa wanafunzi
zaidi ya kuharibu mali zilizokuwa kwenye bweni hilo ambazo thamani yake
haikuweza kufahamika mara moja.
“Tunaendelea kumfuatilia mwanafunzi huyo ili tuweze kumjua na
kumchukulia hatua za kisheria. Hadi sasa bado hatujafanikiwa kumpata
kwani aliandika kwenye sanduku la maoni juu ya dhamira yake hiyo mbaya
ya kuchoma bweni,” alisema Mushongi.
Alisema wanaendelea kuzifanyia kazi taarifa hizo ili wambaini
mwanafunzi huyo kwa hatua zaidi za kisheria. Kikosi cha Zimamoto mkoani
humo, Polisi pamoja na wananchi walifanikiwa kuuzima moto huo hivyo
kuzuia usilete madhara kwa wanafunzi.

0 comments:
Post a Comment