Watu walioathirika ni 53,446, kaya 22,270 zimeathirika wakati hekta 8,138 za mpunga na hekta 7,171 za mahindi zimeharibiwa na mafuriko hayo. Akizungumza na gazeti hili jana ofisini kwake mjini Kibaha, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alisema mahindi hayo yatawasili leo wilayani humo.
“Tunatarajia mahindi hayo yatawasili leo kutoka wakala wa mazao, kisha yatasagwa na wananchi walioathirika watapewa bure,” alisema Ndikilo na kuongeza kuwa tayari magari ya kubeba mahindi hayo kutoka halmashauri kwa ajili ya kuchukua mahindi hayo ya msaada kwa kipindi cha Februari na Machi.
“Pia tumeteua wafanyabiashara sita ambao watanunua mahindi kwa wakala hao kisha kuyauza kwa bei ndogo ili kila mwananchi amudu kununua,” aliongeza mkuu wa mkoa.
CHANZO: GAZETI LA HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment