Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Jamila Shabani akisema kuwa moja ya adhabu wanayopewa watoto ni kuchapwa fimbo hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani
|
Kikundi cha Kisarawe Bomani maarufu kama Kibo katika picha ya pamoja baada ya kupata redio kutoka True Vision hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani |
Kikundi cha Tushirikiane cha Kisarawe wakijadiliana baada ya kupewa Redio na True Vision ili kufuatilia vipindi vya Walinde Watoto hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani |
Na Krantz Mwantepele , Kisarawe
Watanzania
wametakiwa kuwa karibu na watoto wao na kujenga urafiki nao ili kuwawekea
misingi bora ya nidhamu na upendo. Rai hiyo imetolewa na baadhi ya wazazi na
walezi kutoka wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani hivi karibuni wakati wa mdahalo
maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision
production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto.
Katika
mdahalo huo mada mbalimbali zilijadiliwa zikiwemo athari za kuchapa watoto,
matusi pamoja na adhabu kali kwa watoto mfano kuwafukuza watoto nyumbani.
Aidha
washiriki wa mdahalo huo walionyesha kusikitishwa na vitendo vya kuchapa watoto
fimbo kupita kiasi na wengine wakikemea tabia ya baadhi ya wazazi na walezi
kutukana watoto pasipo kuzingatia maadili huku wakiiomba serikali kuwawajibisha
wale wote wanaotukana hadharani bila kujali uwepo wa watoto.
Katika
hatua nyingine, washiriki hao walikemea tabia ya kuwafukuza watoto nyumbani na
kudai kuwa huo ni mwanzo wa kuwaingiza watoto katika matatizo makubwa na
kuongeza idadi ya watoto wa mitaani aidha wamependekeza kuwa ni vyema watoto
wafanyiwe maombi mara kwa mara na kuwashirikisha katika Ibada ili kuwaepusha
kuwa na utovu wa nidhamu.
Kwa
upande wao wanafunzi wa shule ya msingi Kibasila Kisarawe ambao walipata nafasi
ya kuongea na timu ya Walinde Watoto walionyesha kuchukizwa na tabia ya kupewa
adhabu kupita kiasi pamoja na kutukanwa tabia ambayo hufanywa na baadhi ya
walimu na wazazi.
Naye
mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kibasila Kisarawe Debora Mbalilaki
alipendekeza kuangalia uwezekano wa kuwepo na adhabu mbadala badala ya fimbo
kwa wanafunzi.
0 comments:
Post a Comment