Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WATU wanaotoa lugha za uchochezi na vitisho kwenye kijiji cha Magindu
wilayani Kibaha mkoani Pwani, wametakiwa kuacha tabia hiyo kwani
inahatarisha amani kwenye kijiji hicho.
Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho kwenye mkutano wake wa
hadhara, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alisema kuwa amepata
barua inayosema kuwa wafugaji wanaoishi kwenye kijiji hicho watamwaga
damu ya wakulima.
Ndikilo alisema watu hao wanapaswa kuacha vitisho hivyo na hatua kali
za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwani mkoa huo haujafikia hatua ya
watu kuuana kwa ajili ya kugombea ardhi.
“Barua hii inanisikitisha sana na ninawashangaa watu wanaoanzisha
chokochoko za kutaka kumwaga damu kwani Watanzania wanaishi kwa amani na
hakuna haja ya kuharibu amani iliyopo, kisa ardhi,” alisema Ndikilo.
Alisema kuwa hapa kuna historia ya kuishi watu wa aina mbili;
wakulima na wafugaji. “Na mmeishi kwa muda mrefu iweje leo watu waandike
barua kama hiyo ya vitisho,” alihoji Ndikilo.
CHANZO ; HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment