Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (pichani), amedondoka katika kura za maoni zilizorudiwa baada ya kutokea kwa utata katika zoezi hilo.
Dk. Rashid alipata kura 5010 huku mpinzani wake, Mohamed Mchengelwa, akipata kura 6002.
Kabla ya kurudiwa kwa uchaguzi huo, Dk. Seif iliibuka kidedea kwa kupata kura 3831 huku Mchengelwa akipata kura 3560.
Hata hivyo, matokeo hayo yalilalamikiwa na wanachama na kulazimisha uchaguzi urudiwe.
Katibu wa CCM Wilaya ya Rufiji, Mussa Lilio ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo, alisema kulikuwa na kata 13 na vifaa vilifika kwa wakati.
Akitangaza matokeo hayo alisema kuwa kura zilizopigwa ni 11,933 kura zilizoharibika ni 195 na kura halali ni 11,738.
Katika matokeo hayo Dk. Seif alipata kura 5010, Mchengelwa (6002), Juma Rajabu (51), Mohammed Asifu (121), Seif Sare (323) Shabani Matwebe (126) na Seif Mudra (17)
CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment