Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kaimu Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Janeth Ruzangi.
Hatma ya wanakijiji 900 wa Mlingotini, Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wanaotakiwa kupisha mradi wa ujenzi wa bandari ambao hawajalipwa fidia itajulikana Jumatatu ijayo.
Mradi huo ni Mpango wa Uendezaji wa eneo la Ukanda Maalum wa Uwekezaji Bagamoyo (SEZ), lenye ukubwa wa hekta 9,800 ambalo limegusa kata za Zinga na Kiromo kupitia vijiji vya Zinga, Kiromo, Pande, Kondo na Mlingotini.
Katika mpango huo utakaofanyika kwa awamu umetaja maeneo ya uwekezaji yatakayojengwa viwanda na bandari huku eneo lingine likiwa ni kwa ajili ya vyuo, biashara na makazi.
Aidha, kutokana na aina ya uwekezaji hairuhusiwi kuchanganywa ujenzi wa viwanda na makazi ya watu. Wanakijiji walioguswa na mradi, walifanyiwa uthamini mwanzoni mwa mwaka jana kwa ajili ya ulipaji fidia.
Akizungumza na Nipashe Jumamosi kuhusu hatma ya watu hao ambao walipaswa hadi sasa wawe wameshalipwa kutokana na mradi huo kulengwa kuanza mwezi uliopita, Kaimu Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Janeth Ruzangi, alisema kwa sasa wamefikia hatua nzuri. Ruzangi alisema hatua iliyofikiwa ni kuboresha taarifa za uthamini uliofanyika hapo awali.
Alisema uboreshaji huo unatarajiwa kukamilika Jumatatu ijayo ambapo idadi ya wangapi watalipwa itajulikana.
Alisema mara baada ya zoezi hilo kukamilika na vibali kutolewa, ulipaji wa fidia utaanza (bila kusema lini) na unatarajiwa kufungwa ifikapo mwezi Desemba mwaka huu.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mlingotini, Thabiti Kinyogoli aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu kuwa, hivi karibuni walikutana na Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dk. Shukuru Kawambwa, ambaye aliwataka wafungue akaunti kwenye benki ya NMB zoezi ambalo wameshaanza.
Mapema mwaka huu, wakazi hao waliliambia gazeti hili kuwa, licha ya uthamini huo kufanyika mapema na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), kuwaeleza kuwa, tayari fedha ya fidia imeshapatikana.
CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment