Home » » 'Malaria bado tishio kwa watoto'.

'Malaria bado tishio kwa watoto'.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa barani Afrika (Amref) nchini, Rita Norona
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa barani Afrika (Amref) nchini, Rita Norona, amesema pamoja na nchi za Afrika katika kutokomeza malaria, bado idadi ya watoto wanaopoteza maisha kwa ugonjwa huo ni kubwa.
 
Aliyasema hayo alipo-zungumza na NIPASHE kufafanua kuwa kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na Amref, nusu milioni ya watoto walio chini ya miaka mitano hupoteza maisha kila mwaka barani Afrika kwa ugonjwa huo.
 
 Aidha, alisema watoto wapatao 584,000 walipoteza maisha kwa kipindi cha mwaka 2013 pekee, idadi ambayo ni kubwa ukilinganisha na miaka mingine. 
 
“Kasi ya vifo vya watoto ilipungua kwa asilimia 58 mwaka 2000 na kufanya matokeo ya mikakati iliyowekwa na mataifa hayo kufanikiwa kwa kiwango kizuri, lakini takwimu zimekuwa zikibadilika mara kwa mara,” alisema Norona.
 
Aidha alisema makundi yanayoathiriwa zaidi na ugonjwa huu ni pamoja na watoto, kina mama wajawazito na wale wenye upungufu wa kinga mwilini.
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa