Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisanga kata ya Masaki Wilayani Kisarawe Bwana Mohamed Shomoi Mlembe akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu kuzundua Rasmi Shindano la mama shujaa wa chakula 2015 msimu mpya , pamoja na wageni wote waliofika katika sherehe Hizo.
Mgeni Rasmi katika Sherehe za Uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu akizundua Rasmi Shindano hilo, na kuwasihi wakinamama wa Kisarawe wachukue fomu za kushiriki kwa wingi, pia aliwashukuru Shirika la Oxfam kwa kukichagua kijiji cha Kisanga kuwa wenyeji wa Mashindano hayo.
Eluka Kibona, Meneja
Utetezi na Ushawishi wa Oxfam akielezea Historia na Madhumuni ya shindano la Mama shujaa wa Chakula
Kikundi cha sanaa cha Dhahabu wakitoa Burudani ya Shairi wakati Sherehe hizo zikiendelea ambapo maudhui makubwa yalikuwa ni Ushiriki wa mwanamke katika kumiliki Ardhi na Haki zake
Diwani wa wa kata ya Masaki Mh. Pily Kondo Changuhi akishukuru shindano la Mama Shujaa wa Chakula kufanyika katika kijiji cha kisanga na kuwahakikishia washiriki wote kuwa kijiji kipo salama na watashirikiana pamoja kwa mambo yote wakati wa shindano hilo.
Baadhi ya wakazi wa Kisarawe na wageni waalikwa wakiwa katika Sherehe hizo za uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula
Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt. Eugania Kapanabo Akiongea na wageni walikwa katika uzinduzi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambapo aliwashukuru Oxfam kwa Kuanzisha mashindano hayo pia kuona umuhimu wa akina mama kuhusishwa katika kilimo, Umiliki wa Ardhi na Haki zao za msingi na kusisitiza hii ni Njia moja wapo ya kumkwamua Mama kiuchumi.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Kijinsia Ngazi ya Kati Kisarawe Bi. Veronica Sijaona akiwasihi wakina Mama wa Kisarawe kushiriki kwa wingi na kuchukua fomu ili waweze kuungana na akina mama wengune pindi Shindano la Mama Shujaa wa Chakula litakapo anza
Mmoja wa wanakijiji cha Kisanga akijaza fomu ya ushiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Msimu wa 2015
Baadhi ya wanakijiji cha Kisanga wakiwa katika Sherehe hizo za Uzinduzi wa Mama Shujaa wa Chakula
Mh Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Subira Mgalu akiungana na wageni waalikwa pamoja na wanakijiji kusherekea uzinduzi Rasmi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 litakalofanyikia katika kijiji cha Kisanga Kata ya Masaki Wilayani Kisarawe.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh. Subira Mgalu amezindua Rasmi Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 linaloendeshwa na Shirika la Oxfam kupitia kampeni ya Grow lenye lengo la Kumuwezesha Mwanamke katika kilimo na kumkwamua kiuchumi.
Akizungumza katika Sherehe hizo Mh. Subira Mgalu amesema kuwa amefurahishwa na Mashindano hayo kufanyikia wilayani kwake katika kijiji cha Kisanga na kuwasihi wakina mama wengi kuchukua fomu za ushiriki, na kusisitiza kuwa wakina mama wa Kisarawe sio wavivu na kuwataka washiriki ipasavyo ili zawadi na mshindi wa kwanza atokee katika wilaya hiyo. Aliongeza kuwa Shindano hilo linampa mwanamke uwezo wa kutambua haki zake hasa za umiliki wa Ardhi na kuongeza kuwa ni shindano ambalo mshiriki anahitaji kuwa mbunifu,mwenyeuzoefu ili waweze kubadilishana mawazo na kuwa na mbinu za kisasa za kilimo bora.
Nae Mwakilishi kutoka Oxfam Eluka Kibona alitambulisha rasmi kuwa kijiji cha Kisanga ndicho kitakuwa wenyeji wa shindano hilo na kuwa shindano hilo linatarajia kuanza rasmi mwanzoni mwa mwezi wa Nane na kurushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV na zawadi ya Mshindi wa kwanza kuwa Shilingi Milioni Ishirini za Kitanzania ambapo Mshindi atapata kwa njia ya kununuliwa vifaa na zana za Kilimo.
Eluka alizungumzia historia fupi ya shindano hilo ambalo sasa ni mwaka wa nne kuendeshwa na kusisitiza kuwa lengo kuu ni kumfanya mwanamke atambulike katika jamii kuwa nao wakiwezeshwa katika kilimo wanaweza pia wanaweza kumiliki hata ardhi na kuongeza kuwa shindano hilo linawapa wakina mama njia za kisasa za kuendesha Kilimo.
Pia Diwani wa Kata ya Masaki Mh. Pily Chamnguhi aliwasihi akina baba wa Kisarawe kuwaruhusu wake zao na watoto wao wa kike kuchukua fomu kwa wingi na kushiriki katika shindano hilo kwa kuwa hiyo ni moja ya Fursa ambazo watazipata kupitia Shindano la Mama Shujaa wa Chakula.
0 comments:
Post a Comment