VIJANA nchini wametakiwa kuachana na tabia ya kukaa vijiweni bila ya
kujishughulisha na kazi yoyote, badala yake watumie fursa zilizopo za
ujasirimali ili kujiajiri wao wenyewe na kupambana vilivyo na janga la
umasikini.
Wuti huo umetolewa na Ofisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kibaha, Leah
Lwanji kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Hajat Halima Kihemba, wakati wa
mkutano maalumu wa uchaguzi mkuu wa Chama cha Madereva na Wamiliki wa
Pikipiki Kibaha Chamawapiki).
Lwanji, alisema nia na madhumuni ya serikali ni kuhakikisha
inawakomboa vijana wa rika mbalimbali katika kuwasaidia kuwawezesha
kiuchumi ili waweze kupata ajira ambayo itawasaidia kujikimu kimaisha na
kuleta chachu ya maendeleo kwa Taifa.
“Jamani ndugu zangu waendesha pikipiki, kwa upande wangu nawashukuru
sana kwa kuwa na umoja kama huu, lakini sisi kama serikali tupo pamoja
nanyi katika kuwasaidia kwa hali na mali ili muweze kujikwamua kiuchumi,
lakini kitu kikubwa katika kazi zenu lazima muweke nidhamu ya hali ya
juu katika kutunza pesa zenu, hii itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa,”
alisema Lwanji.
Kwa upande wake, Mbunge wa Kibaha Mjini, Silvester Koka, ambaye pia ni
mlezi wa Chama hicho, aliahidi kuwasaidia vijana hao pikipiki katika
Kata 11 za jimbo hilo ili kukuza uchumi wao.
Waliochaguliwa ni Masudi Ngingite (Mwenyekiti), Shabani Kambi
(Katibu), Said Issa (Mweka Hazina), na wajumbe nane wa kamati ya
utendaji.
Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment