CHUO cha Biblia cha Glory of God Ministry cha Kibaha mkoani Pwani kinatarajia kuanzisha mafunzo ujasiriamali kwa waumini wa kanisa na jamii inayokizunguka chuo hicho bila ya kujali imani ili kupambana na umasikini.
Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Mkurugenzi wa chuo hicho, Mchungaji Ernest Mrindoko wakati wa mahafali ya pili ya chuo hicho, ambapo naye alikuwa mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo ya biblia.
Mrindoko alisema mafunzo hayo yataanza kufundishwa mwaka 2015, ambapo wanachuo watapatiwa mafunzo ya miezi mitatu na wasio wanachuo watafundishwa kwa wiki moja hadi tatu.
“Kanisa ambalo linamiliki chuo limeamua kuanzisha mafunzo hayo ambayo yatatolewa hapa kwa waumini na wanajamii wanaozunguka chuo chetu na haitaangalia imani ya mtu bali ni kila mmoja,” alisema Mrindoko.
Alisema lengo ni kuhakikisha jamii inaishi kwenye hali nzuri ya kipato na kuwa na ustawi bora wa maisha kupitia ujasiriamali wa biashara ndogo ili baadaye wawe wakubwa
Chanzo:Habari Leo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment