Home » » WAETHIOPIA 47 WADAKWA MSITU WA MWIDU PWANI

WAETHIOPIA 47 WADAKWA MSITU WA MWIDU PWANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Chalinze. Raia 47 wa Ethiopia wamekamatwa katika Msitu wa Mwidu ulioko eneo la Chalinze wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Wanatuhumiwa kuingia nchini kinyume cha sheria ambapo kati yao, 11 walikutwa wakiwa hawajiwezi kutokana na kutapika hivyo kulazimika kupelekwa katika Kituo cha Afya cha Chalinze kwa uchunguzi na matibabu ya awali.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Athumani Mwambalaswa alisema waliwatia mbaroni baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.
“Tuliletewa taarifa na wasamaria wema kuwa kuna kundi la watu wamejificha kwenye msitu huo na hali zao zinaonekana kudhoofu,” alisema Mwambalaswa.
Hata hivyo, alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa watu hao walitelekezwa na waliokuwa wakiwasafirisha, “Tunaendelea kuwashikilia mpaka hapo Idara ya Uhamiaji itakapochukua hatua nyingine za kisheria,” alisema.
Akizungumzia afya za watu hao, Dk Masam Faustine wa kituo hicho cha Chalinze, alisema zinaendelea vizuri baada ya kuwapatia huduma ya kwanza. “Tulipowafanyia uchunguzi wa awali tulibaini baadhi yao sukari ilikuwa imeshuka sana na wengine walikuwa na malaria,” alibainisha daktari huyo.
Alisema licha ya hali zao kuendelea kuimarika, lakini mpaka jana walikuwa bado wamelazwa kituoni hapo.
Akielezea walivyoingia nchini kutokea Ethiopia, mmoja wa wahamiaji hao ambaye ndiye pekee aliyeweza kuzungumza lunga ya Kiingereza, Dasaliane Nune, alisema wametoka nchini kwao kwa lengo la kwenda Afrika Kusini kutafuta kazi.
Alimtaja raia mmoja wa Ethiopia anayeishi Mombasa, Seleman Said kuwa ndiye aliyewashawishi kwenda Afrika Kusini kutafuta kazi.
Alidai kuwa aliwaambia kuwa huko kuna fursa tofauti na Ethiopia ambako kuna vita vya mara kwa mara.
 Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Pwani Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa