Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
BAADHI ya Wafanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Kisarawe,
Pwani wamesema hawamtaki Meneja wa Misitu, Methew Mwanuo kwa madai ya
rushwa.
Wakizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti wilayani
hapo mwishoni mwa wiki, wafanyabiashara hao walisema wanataka
wabadilishiwe meneja huyo kwa madai ya kusigina utaratibu wa sheria kwa
kuwatoza fedha za vibali na ushuru wa mazao bila kuwapa risiti.
Michael Alphonce, alisema meneja huyo huwatoza faini kati ya sh
200,000 hadi sh 300,000 kila gunia lililozidi kwenye mzigo
unaosafirishwa kitendoi.
“Akisha tupiga faini halafu magunia yaliyozidi anayashusha bila
kutuambia anayapeleka wapi, hivi tunafanya kazi za maendeleo kwa wote au
tunafanya kazi za kuumizana ili wengine wanufaike,” alihoji Alphonce.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, Ali Kombe alisema wamechoshwa na
usumbufu katika utoaji vibali kwani hauna sehemu moja, vitendo vya
rushwa vinavyotishia kuyumba kwa mitaji yao.
Akijibu tuhuma hizo, Mwanuo alisema “Sina la kusema bali natarajia
kukutana na wafanyabiashara hao Julai 17 na wandishi wahabari naamini
mtakuwepo.
“…Kwa sasa nipo likizo siwezi kuzungumza chochote, naomba tuwasiliane baada ya kikao hicho,” alisema Mwanuo.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment